25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kimara Baruti, Tabata zatishiana kuelekea Usiku wa Mabingwa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mabondia wa ngumi za kulipwa Tampera Maurus kutoka Tabata na Waziri Magombana wa Kimara Baruti wametambiana kuelekea pambano lao la Usiku wa Mabingwa, huku kila mmoja akiungana na mashabiki wake kufikisha ujumbe wa kichapo kwa mpinzani.

Pambano hilo linatarajia kupigwa Desemba 26,2023 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam ambapo mabondia mbalimbali watapanda ulingoni siku hiyo.

Akizungumzia maandalizi yake, Magombana amesema ataibuka na ushindi wa kibabe na mashabiki wake watafurahi siku hiyo.

Bondia Tampera Maurus

“Hii ni vita ya Kimara Baruti na Tabata, mpinzani wangu Tampera Maurus ajiandae, safari hii. nitampiga kama amekanyangwa, Nikimgusa tu anapepesuka,” ametamba Magombana.

Kwa upande wake Maurus amesema anakwenda kumfundisha mpinzani wake Magombana ngumi na atampiga kipigo anachokitaka yeye kuhakikisha anamnyamazisha kwa K.O.

“Nitampiga pole pole ninavyotaka mimi,  watanzania wajitokeze kwa wingi nimewaandalia ngumi burudani. Mtaani kwangu kila mtu anajua atakwenda na atakaa VIP kushuhudia,” ametamba Maurus.

Mashabiki wa bondia huyo  Donard Madelanga na  Bobani Mawinda, wamesema  Tabata si sehemu ya wala Bata pekee bali hata  ngumi wanazijua, hivyo mpinzani ajiandae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles