32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara waipa changamoto NCD

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kampuni ya National Commercial Directory ( NCD), imesema inakabiliwa na changamoto kubwa ya wafanyabiashara kutokuwa na uelewa wa kutangaza biashara zao kwenye kitabu chao ili kuwafikia wateja wengi kwa wakati na kujitangaza duniani.

Akizungumza Novemba 8,2023 kwenye maonyesho ya teknolojia za kifedha yanayoendelea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa NCD, Rehema Ahmed amesema kitabu chao kimeorodhesha wafanyabiashara wote Tanzania.

Rehema amesema kwa kutumia kitabu chao wamesaidia kukuza na kurahisisha ufanyaji wa biashara ambapo kimesambazwa kwenye wizara ,taasisi,ubalozini na mahoteli ili kuhakikisha hata mgeni anapata huduma anayotaka.

“Hiki kitabu tunakisambaza ndani na nje ya nchi ili hata mgeni anapokuja hapa anataka kwenda Mwanza anaangalia tu kwenye kitabu anakua anajua afikie hoteli gani na akitaka huduma anazipata bila hata ya kutoka jasho hii inasaidia kutangaza biashara zetu kimataifa lakini tunaitangaza nchi,”amesema Rehema.

Amesema kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia wamefungua kurasa kwenye mitandao ya kijamii lengo kuongeza wigo mpana wa kuwafikia wateja lakini kuongeza hamasa kwa wafanyabiashara kujiunga na kampuni hiyo.

“Tumejiunga na ‘social media’ pia tunataka kufungua na ‘application’ ili tuweze kuwafikia kila mtu ukizingatia sasa hivi dunia ipo kiganjani ndio maana nawashauri wafanyabiashara wengi kuja kusajili biashara zao ili waweze kuwafikia wateja wengi”amesema Rehema

Amesema zaidI ya kampuni 25,000 kubwa, kati na ndogo zimeweza kutangaza biashara zao kwenye kitabu cha kampuni ya NCD.

Ameongeza kuwa wanamkakati wa kuhakikisha wanazifikia biashara zote zilizosajiliwa kisheria bara na visiwani lakini pia kupitia mitandao ya kijamii wameweza kuwafikia watu zaidi ya 600 kwa siku na wanaendelea kuongezeka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles