22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabishara Mkuranga, Kibiti wamsifu Samia uhuru wa kibiashara 

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

Wafanyabiashara wilayani Mkuranga na Kibiti, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuliza dhorobu ya hali ya biashara nchini.

Wamesema kwenye wilaya hizo biashara zinafanyika kwa amani na utulivu bila usumbufu tofauti na miaka ya nyuma.

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti kwenye mkutano kati ya wafanyabishara wa wilaya hizo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara (JWT) inayoendelea na ziara mkoani Pwani yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabishara.

Mfanyabiashara Hassan Kambangwa, amesema wafanyabiashara wilayani humo wananufaidika tangu kuingia kwa utawala wa Rais Samia.

Amesema; “Kimsingi namshuruku Rais Samia kwa kutuletea ugeni uliotupa fursa ya kuzungumza changamoto zinazotukabili, lakini sisi tangu kuingia kwa utawala huu wa Mama Samia tunafaidika nao kwa asilimia kubwa.

Mfanyabiasha huyo ametolea mfano wa mambo wanayofaidika nayo kuwa ni mikopo, uhusiano mzuri na halmashauri lakini pia taasisi mbalimbali za kifedha ziko huru kuwasaidia wafanyabiashara.

Amesema serikali imezingatia suala la amani na utulivu na kwa mikoa mingi ilikuwa inapata changamoto nyingi lakini Wilaya ya Mkuranga wafanyabiashara wako huru na wanafanya biashara bila bugudha.

“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan, tunafanya biashara kwa amani lakini pia tunashukuru ujio huu umefanya tuweze kufunguka yale ambayo yako ndani ya mioyo na tunaamini mtayafikisha,” amesema Kambangwa.

Naye mfanyabishara wa Wilaya ya Kibiti, Salim Juma, amempongeza Rais Samia kwa kuona sekta ya wafanyabishara ni sehemu ya uchumi wa Taifa na kuamua kuungana kwa pamoja kutatua kero zao.

“Ili kuwa na ustawi tumefanikiwa kumpata Rais Samia, ambaye ameona umuhimu wetu na kutambua mchango wetu ndio maana leo viongozi mpo hapa,” amesema Juma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles