26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Skanka kilo 423.54 yakamatwa Kawe

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imekamata kilo 423.54 za bangi iliyosindikwa maarufu kama Skanka maeneo ya Kawe, Dar es Salaam.

Pamoja na kukamatwa kwa dawa hizo, pia mamlaka hiyo imebaini uwepo wa kiwanda cha kutengeneza biskuti zilizochanganywa na bangi katika eneo hilo.

Akizungumza Novemba 8, 2023 jijini Dar es Salaam, Kamishina Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema kufuatia operesheni maalum zilizofanyika kwenye mipaka na fukwe za Bahari ya Hindi ndio zilizofanikisha kukamata dawa hizo za kulevya.

Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kuwa makini na vyakula hasa ikizingatiwa baadhi ya vyakula hivyo hupendwa na watoto.

“Kilo 158.54 zilikamatwa eneo la Kigamboni na Kawe jijini Dar es Salaam zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mabegi ya nguo tayari kwa kusafirishwa, huku kilo 265 zikikamatwa katika matukio tofauti mikoa ya Nyanda za Juu Kusini zikiwa zimefichwa ndani ya magari kwa kuchanganywa na bidhaa nyingine ikiwemo maboksi yenye matunda aina ya ‘Apples’ zikisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam,” amesema.

Aidha mamlaka hiyo imewataka watu wanaojihusisha na utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na skanka kusitisha uzalishaji huo.

Akifafanua tukio hilo, amesema watuhumiwa walikutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengeneza biskuti za bangi.

“Kutokana na operesheni hizo watu 16 wamekamatwa ambapo kati yao sita wamefikishwa mahakamani na 10 watafikishwa baada ya taratibu za kisheria kukamilika lakini pia Mamlaka imebaini maeneo yanayotumika kama masoko ya kusambazia na kuuza Skanka kwenye fukwe ya Bahari ha Hindi,” amesema.

Akifafanua kuhusu Skanka, amesema ni jina la mtaani linaloitambulisha aina ya bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu ikilinganishwa na bangi ya kawaida.

Ameongeza kuwa dawa hiyo ya kulevya hutokana na kilimo cha bangi mseto ambapo asilimia 75 ni bangi aina ya sativa na asilimia 25 ni bangi aina ya indica.

Ameeleza kuwa kiwango cha sumu kilichopo kwenye skanka ni zaidi ya asilimia 45 ukilinganisha na bangi ya kawaida ambayo kiwango chake cha sumu ni kati ya asilimia 3 mpaka 10.

Ameongeza kuwa skanka ina madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji ikiwemo kuamsha na kuzidisha magonjwa ya afya ya akili kwa haraka.

Amebainisha kuwa watu wasio waaminifu huchanganya sanka kwenye vyakula kama vile biskuti, keki, jamu , sharubati , tomato souce pia kwenye sigara na shisha.

Baadhi ya dawa zilizokamatwa

” Lengo la kufanya hivyo ni kurahisisha uuzwaji wa dawa hizo kwa kuficha na kuongeza idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya vyakula hivyo hupendwa na watoto,” amesema.

amesema mamlaka hiyo inaendelea kufanya operesheni dhidi ya wasafirishaji na wazalishaji wa dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha dawa za kulevya haziendelei kuwepo nchini.

” Tunawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya bure ya 119 ambapo taarifa zitapokelewa kwa usiri mkubwa na kufanyiwa kazi.”

Amesema wana mpango wa kuchukua hatua kwa baadhi ya wauza shisha ambao wanachanganya na bangi, kwa wanafanya mchakato wa kuwepo kwa sheria ya kuwabana watu hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles