33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

BMT kuwanoa wanamichezo wanawake

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BARAZA la Michezo la Taifa(BMT), limesema kupitia Tamasha la Michezo la Wanawake maarufu Tanzanite, litatoa elimu ya kuhakikisha kunakuwepo na usawa kati ya wanawake na wanaume michezoni.

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Oktoba 21,2023, likihusisha kongamano kubwa na michezo ya ndani na sanaa ya mapigano (Martial arts) kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Oktoba 18, 2023 jijini, Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha amesema lengo la kufanya tamasha hilo ambalo huu ni msimu wa tatu, ni kuongeza mwamko ushiriki wa wanawake katika michezo.

Neema amesema pamoja na michezo, burudani zitakazokuwepo, watatoa tuzo ya heshima kwa wanamichezo waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa kupitia michezo na anajiimarisha kiuchumi.

“Tutakuwa na kongamano kubwa sana ambalo litatoa mada mbalimbali, mada mojawapo ni suala la kumjengea mwanamke uwezo katika masuala ya uongozi, mada nyingine ni kuwafundisha jinsi ya kubrandi michezo ili kuwaingizia kipato,” amesema Neema.

Ameeleza kuwa kuna watu wengi wamefanya mambo makubwa katika michezo ya wanawake zaidi ya wanaume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles