25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

LHRC yalaani kukamatwa kwa watetezi wa haki za binadamu

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kwa pamoja wamelaani kukamatwa kwa Wakili Boniface Mwabukusi pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu, Dk. Wilbroad Slaa na Mpaluka Said Nyagali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Agosti15, 2023 na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Wakili Anna Henga, amesema Mawakili na watuhumiwa hao wamewaeleza kuwa tuhuma zinazowakabili ni kosa la uhaini ambapo wamehojiwa kwa nyakati tofauti katika vituo vya Polisi.

“Hata hivyo, taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Agosti 12, 2023 ilieleza kwamba Boniface Mwabukusi na Mpaluka Nyagali walikamatwa saa nane na nusu usiku wa tarehe 12/08/2023 maeneo ya Mikumi Morogoro.

“Taarifa hiyo inaeleza kuwa ni watuhumiwa waliandaa na kutoa maneno ya uchochezi. Wakili wa Dk. Slaa naye alitueleza kwamba Dk. Slaa alikamatwa Agosti 13, 2023 na kupelekwa kituo cha Polisi Mbweni, baadaye alienda kupekuliwa nyumbani kwake na hatimae alipelekwa kituo cha Polisi Oysterbay.

“Akiwa kituo cha Polisi Oysterbay, Dk. Slaa alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi lakini baadaye tuhuma zikabadilishwa na kuhojiwa tena kwa tuhuma za uhaini, kama ilivyofanyika kwa Wakili Mwabukusi na Nyagali kutokana na taarifa ya Jeshi la Polisi pamoja na ile ya mawakili wa watuhumiwa, ni dhahiri kwamba watuhumiwa walikamatwa kwa tuhuma za uchochezi lakini tuhuma za uhaini walipewa kwenye vituo vya Polisi, hii ni kinyume na kanuni za kimataifa za upelelezi wa makosa va jinai,” amesema Henga na kuongeza:

“Itakumbuklwa hivi karibuni wakili Mwabukusi pamoja na wanaharakati wengine wa haki za binadamu akiwemo Wakili Peter Madeleka ambaye amefutiwa makubaliano ya hati ya kukiri kosa, wamekuwa wakishiriki katika mijadala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongea na vyombo vya habari kuhusu mkataba wa uwekezaji wa bandari ulioingiwa kati ya Serikali ya Jamhuri va Muungano wa Tanzania na Emirati ya Dubai huku wakieleza mapungufu kadhaa ya mkataba huo ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri kwa Serikali,” amesema Henga.

Amesema wao kama mashirika ya Haki za Binadamu wanaamini kwamba Watetezi wa Haki za Binadamu wana haki ya kutoa maoni kuhusu jambo lolote katika nchi yetu ikiwemo kuhusu maboresho ya mkataba wa bandari na hawastahili kupata vitisho au kukamatwa kwasababu ya kutumia uhuru wao uliopo kikatiba na unaolindwa na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles