24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Fisi mwenye kichaa alivyoacha ulemavu wa kudumu Ngorongoro

*Mwanamke apoteza jicho, masikio, mikono na fuvu

“Aiomba Serikali kuwahamisha haraka

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

“Nimepoteza masikio, jicho, viganja vya mikono yangu miwili na fuvu la kichwa wakati nikikabiliana na fisi ili asiweze kula mifugo yangu katika hifadhi ya Ngorongoro, sasa nimebaki na ulemavu huu wa kudumu,” ni maneno ya Rose Kapande (50) mkazi wa kijiji cha Esapai kata ya Nainokanoka wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Akizungumza kwa unyinge na simanzi kubwa, mama huyu anasema kuwa alifikwa na mkasa huo mwaka 2018 fisi huyo anayetajwa kuwa na kichaa cha mbwa pia akifanikiwa kuua ng’ombe wanne.

Rose aliyekuwa akiishi peke yake ndani ya boma baada ya kutalikiana na mumew,e ni mmoja wa waathirika wa matukio ya kuvamiwa na kisha kushambuliwa na wanyamapori.

Kutokana na madhila hayo Rose ambaye ni mama wa watoto tisa, anaiomba Serikali kumpatia msaada ikiwa ni pamoja na kuhamishwa kutoka katika eneo hilo ambalo limekuwa likicha maisha ya wananchi wengi shakani kutokana na kuwamiwa na wanyama wakali mara kwa mara.

Matukio mbalimbali ya vifo vitokanavyo na wanyapori kwa binadamu na wakati mwingine kusababisha ulemavu yanatajwa kuchangiwa na ongezeko hili la binadamu na mifugo.

Ikumbukwe kuwa eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro linatajwa kama eneo la Uhifadhi Mseto, masuala matatu yakifanyika kwa maana ya uhifadhi, uendelezaji wa jamii inayoishi katika eneo hili na utalii wakiruhusiwa binadamu jamii ya wafugaji, mifugo, ng’ombe, mbuzi na kondoo kuishi pamoja na wanyamapori.

Hata hivyo, utaratibu huo baadhi ya nyaraka zinaeleza kuwa ulikuwa ni sehemu ya majaribio kuona kama inawezekana ukilenga kutizama uwiano wa mambo matatu kwa maana ya uhifadhi maendeleo ya jamii na utalii.

Changamoto iliyopo sasa kwa wakati huu ni idadi ya watu kuongezeka kutoka 8,000 hadi kufikia 100,000 hii ni sawa na kusema kwamba ongezeko la watu ni mara 10 zaidi, wakati hifadhi hii ikianzishwa, mifugo ikiongezeka hadi kufikia milioni moja kutoka 260,000.

Ongezeko la idadi ya watu na wanyama limechochea kupungua kwa eneo la malisho pamoja na muingiliano wa wanyamapori na wananchi ambao pia umechangia uwepo wa muingiliano wa magonjwa yanayotoka kwa mifugo, wanyamapori na binadamu.

Mamlaka zinasemaje

Mamlaka ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kupitia Naibu Kamishna Mkuu wake, Elibariki Bajuta amekiri kutokea kwa matukio ya namna hiyo katika eneo la hifadhi na kwamba tukio la mama huyo Serikali ilifanya jitihada za haraka kuokoa maisha ya mwanamke huyo kwa kuhakikisha anapata matibabu yanayostahili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles