29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Asas akerwa na wanaochukizwa kwa yeye kusaidia jamii

Na Raymond Minja, Iringa

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Abril Asas ameonesha kuchukizwa na kutoridhishwa na Baadhi ya vikundi vya wanasiasa ambao wamekuwa hawafurahishwi na na namna anavyojitoa kusaidia jamii.

Amesema amekuwa akifanya hivyo kwa moyo wa kujitolea na siyo ajenda za kisiasa kwani hana mpango wa kugombea Ubunge kama baadhi wanavyosema.

Asas ameyasema hayo Mei 29, 2023 wakati akizungumza na wafanyabiara wadogowadogo (Machinga) wa Manispaa ya Iringa ambao Machi, Mwaka huu waliamishwa katikati ya Mji na kutengewa eneo la Mlandege kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

“Kumekuwa na chama kinanisema kila kukicha kwa kuwasaidia watu, hivi ndugu zangu tumefika huko, mimi nafanya haya kuwasaidia ndugu zangu hii ni sadaka na nitalipwa na Mungu,” amesema Asas.

Licha ya wamachinga hao kuhamia eneo walilopangiwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa umeme, maji na mitaji.

Katika kutatua hayo Asas ameutaka Uongozi wa shirikisho la Machinga kupeleka gharama zote hadi kufanikisha kuwekwa kwa umeme na maji katika eneo hilo pia amewaahidi kuwapatia Mtaji kwa ajili ya kunusuru biashara zao.

“Niwaombe viongozi leteni mapendekezo yeno haya ya umeme, maji tujue ni gharama kiasi gani ili tuwasaidie ila wale ambao mitaji yao imeyumba tuleteeni tutawasaidia mitaji yao,’ amesema Asas.

Ikumbukwe hii si mara ya kwanza Asas kusaidia kundi hili kwani aliwahi kuwachangia Sh milioni 100 ambapo Sh milioni 50 zilitumika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara zao na Sh milioni 50 kwa ajili ya mfuko wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles