27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ziara ya Chongolo yamnufaish Balozi wa nyumba 10

Na Raymond Minja, Iringa

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mwenyekiti wa shina (Balozi) namba saba, Rose Nzelemera katika Kijiji cha Ilambilole Kata ya Kising’a iliyopo Jimbo la Isimani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Chongolo ameongoza harambee hiyo jana wakati wa ziara katika ubalozi huo ambapo viongozi mbalimbali wa CCM walioambatana naye kwenye ziara hiyo walichangia vifaa vya ujenzi na fedha taslimu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.

Ameagiza ujenzi wa nyumba hiyo uanze haraka ili kiongozi huyo ahamie na kwamba ikishakamilika atahudhuria sherehe ya uzinduzi.

Rose anaishi katika nyumba ya kupanga jambo ambalo liliwafanya viongozi wa CCM kumchangia ili apate nyumba yake binafsi kwa sababu kiongozi wa shida ndio mtu anayekipigania chama.

Chongolo yupo Iringa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa chama ngazi za mashina, pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi akiambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Sofia Mjema na Katibu wa NEC, Oganizesheni, Issa Gavu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles