24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kigoma yafanya vizuri ukusanyaji mapato ya Madini

Na Editha Karlo, Kigoma

MKOA Kigoma umetajwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na madini kutoka kwa wachimbaji wadogo ikielezwa kuwa marekebisho ya sheria na mazingira wezeshi yamechangia katika hilo. 

Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Kigoma wakifuatilia semina kuhusu uchimbaji madini salama inayofanyika mjini Kigoma.

Hayo yamebainishwa Mei 30, 2023 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini nchini, Mhandisi Yahaya Semamba wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wachimbaji wadogo wa madini na kusema kuwa serikali imeweka mazingira wezeshi ambayo yanawafanya wachimbaji hao kufanya shughuli zao kwa tija.

Amesema kumarishwa kwa shughuli za utendaji kwa wachimbaji wadogo kumewezesha wachimbaji hao kuongeza makusanyo ya pato la serikali katika sekta ya madini kufikia asilimia 40 na mpango wa serikali ni kuwezesha wachimbaji wadogo kuingiza asilimia 50 ya pato la Taifa.

“Mkoa wa Kigoma umeweza kufanya vizuri katika sekta ya madini kwa mwaka huu wa fedha unamaolizika mwezi Juni kwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 1.3 katika lengo la kukusanya Sh bilioni 1.6 ambapo lengo la serikali ni kukusanya kiasi cha Sh bilioni 822 kwa mwaka huu wa fedha kwa sekta nzima ya madini,” amesema Mhandisi Semamba.

Katika hatua nyingine, Mhandidi Semamba amewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani Kigoma  kuunda umoja na ushirikiano na wachimbaji na wanunuzi wa madini kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu ili kuimarisha soko la madini nchini. 

Mhandisi Semamba amesema kuwa mwaka 2017 serikali iliifanyia marekebisho  ya sheria ya madini sambamba na kuondoa tozo na kodi mbalimbali ambazo zilikuwa zinalalamikiwa lengo likiwa kuweka mazingira wezeshi kwa watu wa nje kufanya shughuli za madini lakini kutumia masoko yaliyopo nchini Tanzania kwa ajili ya kuuza madini yao.

Awali, akizungumza kabla kufunguliwa kwa mafunzo hayo Katibu Msaidizi wa Chama cha wachimba madini mkoani Kigoma (KIGOREMA), Boaz Mkohozi alisema kuwa wanashukuru serikali imeanza kurekebisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya madini ili kuwezesha wachimbaji na watu wanaoshughulika na madini kazi zao kuwa na tija. 

Hata hivyo, alisema kuwa bado wachimbaji wadogo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya vifaa duni katika kazi zao sambamba na changamoto ya upatikanaji wa mikopo kutoka taasisi za fedha ili wanunue zana bora na za kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles