25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha APR akubali upinzani wa Yanga

slide-image-2NA SUZANA MAKORONGO (RCT)

KOCHA Mkuu wa timu ya APR ya Rwanda, Nizar Khenfir, amesema anatambua umuhimu na ugumu wa mchezo wa leo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

APR ambao waliwasili nchini juzi kwa maandalizi ya mchezo huo, wanahitaji matokeo ya ushindi ugenini ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele baada ya kupoteza mchezo wa awali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Khenfir alisema anategemea upinzani mkali kutoka kwa wenyeji wao Yanga, lakini wamejipanga kuibuka na ushindi baada ya kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa awali ambapo walifungwa mabao 2-1 nyumbani.

“Mchezo wa leo si rahisi kwa upande wetu kwani tunatakiwa kubadili matokeo ya kufungwa mchezo wa awali kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Yanga,” alisema.

Alisema wana uhakika wa kuwafunga Yanga nyumbani kwani hawaoni sababu ya kushindwa kufanya hivyo, kwa kuwa wapo tayari kutokana na kikosi kuimarika kila idara.

Yanga ambao waliiondosha Cercle de Joachim katika hatua ya awali ya Klabu Bingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-0, ikiwa ni ushindi wa 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani, wanahitaji matokeo ya ushindi au sare yoyote ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Timu itakayofanikiwa kuvuka raundi ya kwanza kati ya Yanga na APR, itakutana na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri au Libolo FC ya Angola.

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles