27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Magufuli amkabidhi Ridhiwani gari la wagonjwa

Pg 3Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

RAIS John Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kwa Hospitali ya Wilaya ya Chalinze ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kwa niaba ya Rais Magufuli, Katibu Mkuu wa Ikulu, Peter Ilomo, alikabidhi gari hilo Ikulu, Dar es Salaam jana kwa Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete.

Taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya Ilomo kukabidhi gari hilo, alisema Magufuli amelitoa ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake.

“Hivyo nawaomba viongozi wa Jimbo la Chalinze walitumie gari hili kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo,” alisema Ilomo.

Alisema mbali na msaada huo wa gari hilo kwa Wilaya ya Chalinze, pia magari mengine mawili yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.

Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa Chalinze, Ridhiwani, alimshukuru Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kuwa litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa msaada huu. Utendaji kazi wake unaungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali hivyo nawaomba Watanzania tuzidi kumuombea kwa Mungu,” alisema Ridhiwani.

Naye Dk. Nasoro Matuzya alisema gari hilo limekuja wakati mwafaka kwa kuwa linatekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) hasa lengo namba nne la kupunguza vifo vya wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmshauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, alisema gari hilo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo na litasaidia kuwatoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na kuwafikisha katika Hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa kupata huduma za afya kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles