33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali iweke mazingira ya Maofisa habari kutoa taarifa-Marenga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ugumu wa Mwanahabari kupata taarifa anazozitaka kutoka katika Taasisi za Serikali na Umma, unasababishwa na kutokuwepo kwa sheria inayowasukuma maofisa kutekeleza utaratibu huo.

Akizungumza juzi jiji Dar es Salaam, James Marenga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa MISA – TAN amesema, hakuna sheria inayoeleza iwapo ofisa wa serikali asipotoa taarifa, nini kitafuata.

Kauli ya Wakili Marenga ambaye ni wakili wa kujitegemea, imetokana na kauli ya Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali aliyowataka wanahabari kwenda kupata taarifa wanazozitaka kutoka kwa maofisa habari wa taasisi za serikali na iwapo watakosa basi waende kwa ‘mabosi’ wao.

Msigwa alitoa taarifa hiyo Julai 19, 2022, wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Utekelezaji wa Miradi ya Maji ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Dodoma.

“Wakati mwingine waandishi tumekuwa tukilalamika, sio lazima umpate mkuu wa taasisi hiyo, afisa habari amewekaa pale kwa ajili ya kukusaidia,” amesema Msigwa.

Hata hivyo, Msigwa amesema, kutokana na kutokuwepo msukumo kwa maofisa habari ama wakuu wa idara kutoa taarifa, wanahabari wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kupata taarifa hata kama wamefuata utaratibu wa kuomba taarifa hizo.

“Tunaweza kuzungumza kila siku wanahabari wapewe ushirikiano, lakini tatizo linabaki kuwa, maofisa ama wakuu wa idara hata wasipotoa taarifa walizoombwa, sheria haielezi wafanywe nini,” amesema Wakili Marenga na kuongeza:

“Hili ndio linalotusukuma kutaka yafanyike mabadiliko ya sheria za habari kwa kuwa, sheria hii ilivyo haimchukulii hatua ofisa aliyeshindwa kutoa taarifa kwa mwanahabari,” amesema Wakili Marenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles