27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Benki ya NMB yamwaga neema Shule tano Wilaya ya Temeke

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digitl

Benki ya NMB jana ilikabidhi msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya milioni 39 kwa shule tano za Temeke huku iksisitiza dhamira yake ya kuendelea kusaidia mipango ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini kote.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 600, madawati 100 na meza 50 yatakayonufaisha Shule ya Msingi Chem Chem, Shule ya Msingi Azimio, Shule ya Msingi Mtoni, Shule ya Msingi Magurumbasi na Shule ya Sekondari Kibasila.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika Sekondari ya Kibasila, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisema jitihada za benki hiyo zinalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu.

“Serikali imefanya kazi kubwa ya kuweka miundombinu ya sekta ya elimu. Shule nyingi mpya zimejengwa na Serikali ya awamu ya sita. Kama benki, tunaona ni muhimu kuunga mkono juhudi za kuinua sekta hii ndomaana tumejikita kutoa vifaa vya shule nchi nzima,” alisema

Aliongeza, “Kama benki, tunatoa asilimia moja ya faida yetu kila mwaka kusaidia sekta ambazo tuimezipa kipaumbele katika mkakati wetu wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambao unalenga sekta kama vile afya, elimu na dharura. Kama sehemu ya mpango wetu wa CSR, leo tunakabidhi bidhaa zenye thamani ya Sh milioni 39 na tunaamini hii itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zitakazonufaika,” amesema.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave alisema msaada huo umekuja wakati muafaka hasa wakati huu ambapo wilaye yake imeeanza kutekeleza kampeni yake ya ‘Boresha vya Kale’ ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kukarabati shule kongwe wilayani humo.

“Serikali imeanza kujenga shule mpya kote nchini ila siai mama wilaya, tumeona  ni wakati muafaka wa kuboresha shule kongwe ili zisibaki nyuma zikiwa katika hali mbaya ndiyo maana tukaja na kampeni hii. Tunaishukuru Benki ya NMB kwa kuunga mkono juhudi zetu na tunaamini msaada wao utafanikisha kampeni yetu,” amesema Kilave.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hassan Rugwa aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuunga mkono wilaya hiyo na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele na bidhaa nyingi zinalenga watu wa ngazi ya chini.

“Kuna kambuni nying katika sekta ya kibenki na fedha lakini Benki ya NMB ni ya kipekee. Hivi karibuni, benki ilitangaza bidhaa yake ya mkopo wa elimu ambayo itanufaisha watoto kutoka familia masikini. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru NMB kwa kuendelea kutuunga mkono,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles