Na MWandishi Wetu, Mtanzania Digital
Ziara ya Kijiji kwa Kijiji imemfikisha Waziri wa Nishati, January Makamba kwenye Kijiji cha Kilando Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na kuzungumza na Wananchi mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara ambapo walifanikiwa kuwasilisha kero zao, Miongoni mwa kero zilizowasilishwa ni pamoja na kuwepo kwa gharama kubwa za kuunganishiwa umeme.
Waziri Makamba kwenye kulijibu hilo amesema: “Ndugu zangu gharama ya vifaa ni kubwa sana, na kwa sasa mfano tu bei ya Mita ni 320,000, Bei ya Waya kwa mita 1 ni 57,000 na kuna sehemu zina urefu zaidi ya mita 30 na bado hakuna Mtanzania anachajiwa gharama ya huduma (Service Charge) ambayo yote hayo ukiamua kupiga hesabu ni zaidi ya Laki sita za Kitanzania.
“Makamba ameendelea kwa kusema’kwa Mtanzania sasa hivi wa Mjini analipa 320,000 na wa Kijijini 27,000 tu, hizi gharama ukizisema watu wanaweza kuona nyingi lakini kwenye utendaji ni ndogo, Tunahitaji Shirika letu la Tanesco likue na lijiendeshe hivyo sisi kama Watanzania tuna wajibu huu wa kufanikisha hili,” amesema Makamba.