24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

DC Haule amshukuru Prof. Muhongo kuhimiza Sensa

Na Shomari Binda, Musoma

MWENYEKITI wa Kamati ya Sensa Wilaya ya Musoma ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Khalfan Haule amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, kuunga mkono zoezi la Sensa.

Haule amesema hayo wakati akizungumza kwenye tukio la kufungwa kwa mafunzo ya siku 21 ya wakufunzi wa Sensa mkoa wa Mara kwenye ukumbi wa Buhare CDTI.

Amesema kwa upande wa jimbo la Musoma vijijini mbunge wa jimbo hilo yupo bega kwa bega na serikali kuona zoezi hilo linafanikiwa.

Mwenyekiti huyo wa Sensa wilaya ya Musoma amesema Prof. Muhongo amechukua jukumu la kuchapisha vipeperushi vitakavyosambazwa jimbo zima kwaajili ya uhamasishaji.

Amesema wakati serikali ikiendelea na jitihada zake za zoezi la Sensa viongozi kwenye maeneo yao wanapaswa kuunga mkono ili kufanikiwa zaidi.

“Tunamshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kwa kuwa bega kwa bega katika kufanikisha zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Lakini tunapokwenda kuwapata makarani wa sensa tuangalie kwa makini washiriki maana wapo waliokuwa nje wakati wa zoezi la anuani za makazi,” amesema Haule.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kuelekea zoezi la Sensa imeandaa kampeni maalumu ya zoezi hilo itakayoanza Julai 30.

Licha vipeperushi hivyo vikundi vya burudani vimeandaliwa kwa ajili ya kufanya uhamasishaji katika kuzunguka Kata 21 na vijiji 68.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles