29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Global Education Link yawataka wanafunzi kutokata tamaa kujiendeleza kielimu

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

WANAFUNZI nchini wametakiwa kutokata taama katika kujiendeleza kielimu badala yake wafike katika banda la Wakala wa Vyuo Vikuu vya Nje ya nchi la Global Education Link (GEL) ili kupata msaada wa kimasomo.

Akizungumza naMtanzania Digital katika maonesho ya 17 ya elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, Meneja wa Tawi wa Chuo Kikuu cha Global, Micky Musa amesema kwa mwaka huu jukumu kubwa la chuo ni kuhakikisha kinatatua changamoto za wanafunzi wanaohitaji kujiunga na vyuo kikuu vya ndani na nje ya nchi.

Amesema wapo wanafunzi waliokata tamaa za kushindwa kujiuunga na vyuo vikuu kwa sababu mbali mbali ikiwemo ya uchumi.

“Sisi GEL tupo hapa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi ambao wameshindwa kupata msaada wa kielimu, sisi GEL tuna vyuo vikuu vingi nje ya nchi na walimu waliobobea wenye uzoefu wa kutosha,” amesema Musa.

Amefafanua zaidi kuwa kwasasa GEL kimejiunga na Benki ya Amana kwa lengo la kuwakopesha wazazi mkopo usiokuwa na riba kwa asilimia 50 hadi 70 ili kuweza kumsaidia mwanafunzi.

Amesema katika mkopo huo mzazi atalipa ndani ya miezi 8 huku mtoto wake akiendelea na masomo.

“GEL ni tofauti na vyuo vingine kwani mzazi anasaidiwa kutafuta chuo pamoja na usafiri na sehemu husika anayoenda kusoma, mzazi wa mwanafunzi anapokuja katika chuo chetu sisi tunamshauri mwanafunzi kozi inayofaa kuweza kusomea lakini shuhuli zote zinazomuhusu mwanafunzi ikiwa ni pamoja visa, udahili tunalisimamia wenyewe,” amesema.

Alisema kwa wanafunzi wataokafika katika maonyesho hayo akiwa na matokea yake ya kidato cha nne au cha sita anapatiwa udahili akiwa hapohapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles