22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo cha Takwimu Afrika Mashariki chajivunia upekee wake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimewahimiza Watanzania kujiunga na chuo hicho kwa kuwa ndiyo pekee kinafundisha takwimu rasmi nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Eusebius Mwisongo wakati akizungumza na Mtanzania Digital katika maonyesho ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

“Tunawakaribisha Watanzania kujiunga na chuo chetu kwa mafunzo ya takwimu, lakini pia tuna programu ambazo hazifundishwi na vyuo vingine ikiwemo Data Sayansi inayotolewa na sisi tu.

“Hivyo programu zetu ni zakipekee ambazo huwezi kuzipata chuo kingine ndani ya nchi yetu, hivyo ndiyo sababu tunahimiza Watanzania kujiunga na chuo hiki,” amesema Mwisongo.

Amesema chuo hicho kinazalisha wataalamu wa takwimu ambao wengi wao wanatumika katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Watalaamu wetu pia wanatumika katika nchi wanachama 19 zinazoongea Kiingereza barani Afrika. Ndani ya nchi kimesaidia kutoa mchango mkubwa wa watumishi ambao wengi wao ndio wanatumika kukusanya na kuchakata takwimu kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).

“Hata kwenye zoezi la Sensa la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu chuo chetu kinashiriki kutoa mafunzo na hata baadhi ya wahitimu wetu wamepata nafasi za kusimamia zoezi hilo kwasababu wameonekana wanafaa,” amesema Mwisongo.

Aidha, amewasihi Watanzania kufika chuoni hapo ili kuangalia programu zinazowafaa kwa ajili ya kujinoa kitaaluma.

Baadhi ya programu hizo ni Shahada ya Takwimu Rasmi, Shahada ya Takwimu za Kilimo na Uchumi, Shahada ya Takwimu za Biashara na Uchumi na Data Sayansi.

Nyingine ni Shahada ya Uzamili katika Takwimu Rasmi na Shahada ya Sayansi katika Takwimu za Kilimo. Pia chuo kinatoa mafunzo ya takwimu katika ngazi Cheti na Diploma.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kinapatikana katika eneo la Changanyikeni jirani na chuo kikuu cha Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles