Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
TANZANIA ni kati ya nchi chache za Afrika ambazo zimebarikiwa kuwa kitega uchumi cha bandari.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wamekuwa wakitafasri bandari kama moja ya lango kuu la uchumi wa nchi.
Kwani tumeona nchi kadhaa ambazo zimefanikiwa kutokana na kutumia vizuri raslimali yake ya bandari.
Bandari ya Dar es Salaam ni moja ya bandari kubwa na tegemeo siyo tu Tanzania bali Afrika Mashariki na Kati.
Kwani uwepo wake umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kutumainiwa na nchi nyingine katika kupokea na kusafirisha mizigo.
Hata hivyo, ukweli ni kwamba bandari hiyo bado ufanisi wake hauendani na matarajio ya wengi hatua ambayo inatafasriwa kama inachelewesha manufaa kwa taifa.
Changamoto kubwa katika hilo inaelezwa kuwa ni kutokana na kuwapo kwa Kampuni ya kuhudumia makontena Tanzania (TICTS)Â ambayo imekuwa changamoto.
Wadau mbalimbali wamesikika wakisema kuwa hakuna haja ya kwa kampuni hiyo kuongezewa mkataba baada ya kumalizika ile wa awali.
Chama cha ACT Wazalendo kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa, pia kimeitaka Serikali isitishe nyongeza ya mkataba huo kwa sababu mbalimbali ambazo kimeziainisha.
Ucheleweshaji wa ushushaji na kuondosha mizigo.
Chama hicho kinasema kuwa moja ya sababu kubwa ni malalamiko ya muda mrefu ya wafanyabiashara na waagizaji, ambao wamekuwa wakibeba mzigo wa gharama za uchelewaji wa kufunga meli na kuondosha mizigo.
“Mfano Chama wa Mawakala wa Forodha (TAFFA) wamekuwa wakilalamika miaka nenda rudi kuhusu TICTS kuwa na ufanisi mdogo na kusababisha ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.
“Malalamiko haya yamethibitishwa na repoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) karibu kila mwaka. Mfano ripoti ya CAG ya mwaka 2020/21 inaonyesha kuwa kuna ucheleweshaji wa ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam jambo linasababisha malalamiko ya wateja na kuathiri ufanisi wa utendaji wa bandari.
“CAG alionyesha meli za mizigo na mafuta zinachukua wastani wa siku tatu hadi nane kupakua mizigo kinyume na mipango ya mamlaka ya bandari ya kuhakikisha inapunguza hadi kufikia siku mbili,” kinabainisha chama hicho na kuongeza kuwa:
“Ucheleweshaji huu na utendaji hafifu wa TICTS unasababisha meli kukaa muda mrefu bandarini na kunaathiri utendaji na ufanisi wa bandari kwa ujumla,” kinaeleza chama hicho.
Ikumbukwe kuwa Aprili mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa agizo kwa kampuni hiyo kuimarisha utendaji kazi wake ili kuondoa kero ya ucheleweshaji wa mizogo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kama hiyo haitoshi, hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan aliikosoa hadharani Bandari ya Dar es Salaam kwa kukosa ufanisi na kumfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi, na kumteua, Plasduce Mbossa ambaye ameahidi kuongeza ufanisi wa bandari.
Kushindwa au kutokua na utayari wa kuwekeza ipasavyo kwenye miundombinu ya bandari (equipment, logistics corridor, etc.).
Kwa mujibu wa mkataba, taasisi hiyo ilitakiwa iwe inawekeza katika kuimarisha eneo la kuweka na kupokea makontena ili kukuza huduma za kuhudumia makontena kwa asilimia 37 kwa mwaka lakini hilo halijatekelezwa.
Madhara kwa nchi:
Kusuasua huko kumesababisha kero na gharama kwa wafanya biashara na waagizaji – ambao ndio wanobeba mzigo wa ucheleweshaji na utendaji mbovu wa TICTS – kama ambavyo wamekuwa wakilalamika miaka yote 20 ya mkataba wa TICTS.
Aidha, bandari ya Dar es Salaam inapoteza ushindani wa kibiashara kwa nchi nyigne – mathalani bandari ya Mombasa.
Takwimu zinaonyesha wakati bandari ya Dar es Salaam ina kila faida ya kijiiograofia, mwaka 2021 iliingiza kontena 606,169 tu mbacho ndio kiwango cha juu ilichowahi kufikia; wakati Bandari ya Mombasa iliingiza kontena million 1.4 mwaka 2019, na inapanga kufikisha kontena million 2 mwaka huu na kuwa bandari kitovu kwenye Pwani ya Afrika Mashariki.
Kudumaza kukua kwa bandari ya Dar es Salaam ambayo ienelenga kuongeza mzigo wa kontena asilimia 37% kwa mwaka.
TICTS imeshindwa kabisa kwenye hili – kati ya mwaka 2020 na 2021 TICTS haikuweza kufikia ongezeko la hata asimilia moja (ongezeko lilikua 0.8% tu).
Kuhatarisha maslahi ya taifa:
Takriban asilimia 90 ya biashara za Tanzania zinapita bandari ya Dar es Salaam.
Vile vile ndio bandari inayopendelewa zaidi na nchi jirani (DRC, Uganda, Rwanda, Burundi, Malwai, Zambia, n.k.) kwa sababu ya nafasi yake ya kipekee ya kijiografia.
Dhima ya serikali kuipa sekta bianfsi ushiriki kwenye mashirika ya umma ni kuchochea maendeleo na kulinda maslahi mapana ya taifa.
Kwa miaka 20, TICTS imeshindwa kufanya yaliyotarajiwa kwenye matakwa ya mkataba na utendandi wake umekua ukilalamikiwa miaka yote.
Kuendelea kuikumbatia ni kuhujumu uchumi wa taifa:
2017 Rais wa Awamu ya Tano Hayati, Dk, John Magufuli aligaiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kupitia upya mkataba wa TICTS akisema hauna maslahi kwa taifa.
Huku mwaka 2008 Bunge lilipitisha azimio lililoiagiza serikali kubatilisha nyongeza ya mkataba wa TICTS.
Nini Kifanyike:
Serikali isitishe nyongeza ya mkataba na TICTS, kwenye kutoa zabuni mpya serikali ifanye uchambuzi wa kina na kutafuta kampuni za kimataifa zenye competitive track record in port operations, watakaoleta ufanisi, na wenye network kubwa duniani kuongeza traffic ya cargo kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa manufunaa ya taifa.