28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

BASATA watoa pongezi kwa Waandaaji na Wadhamini wa Miss Tanzania 2022

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

BARAZA la Sanaa la Taifa(BASATA) limewapongeza Waandaaji na Wadhamini wa Shindano la Miss Tanzania 2022 kwa kukamilisha mchakato wa kumpata Miss Tanzania 2022 kwa viwango vya juu.

Shindano la Miss Tanzania lilifanyika Mei 20, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, nakushuhudia, Halima Kopwe, akiibuka mshindi na kukabidhiwa gari yenye thamani ya Sh milioni 40 na fedha Sh milion 10 kwa ajili ya maandalizi ya shindano la Miss World.

Akizungumaza na Wandishi wa Habari ljijini Dar es Salaam leo Alhamisi Juni 16, 2022, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa, Matiko Mniko, amesema wamefurahishwa na uendeshaji wa shindano hilo ulivyokwenda.

“Kwa niaba ya Serekali niwapongeze waandaaji wa shindano hili ambao ni The Look Campany Limited, pamoja na wadhamini ambao ni Star Times, kwa kuandaa shindano lenye kiwango cha juu na kutoa zawadi zenye thamani ya kuheshimisha tasnia ya urembo hapa nchini, sisi kama Basata tunawatunuku vyeti vya pongezi na baruau,” amesema Mniko.

Nae, Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Azama Mashango, amesema wanafurahi kwa kuwa Basata imetambua kazi yao na kuomba waendelee kuwashika mkono ili kukuza tasnia ya urembo.

Kwa upande wa waandaaji Afisa Masoko wa Star Times, David Malisa amesema tayari wameanza kujiandaa kwa msimu mpya wa shindano hilo kwa sababu wanataka kufanya vizuri zaidi.

“Tunashukuru kwa pongezi za Basata tumezipokea na tuna ahidi kuboresha zaidi shindano hilo tumejipanga kwa msimu ujao tutaanzia ngazi ya mkoa, kanda mpaka Taifa ili kuboresha zaidi,” amesema Maliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles