Na Renatha Kipaka, Muleba
Wazazi na walezi wilayani Muleba mkoani Kagera wameshauriwa kuwaambia ukweli watoto wao ili wajue jinsi hali halisi ya mabadiliko pamoja na utandawazi katika jamii ulivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Humuliza, Victor Nestory wakati akizungumza na Mtanzania Digital jana.
Mabadiliko ya utandawazi katika jamii yanaendana sambamba na mabadiriko ya mwili kwa watoto hivyo wazazi tuwe wawazi ili wajue kinacho endelea.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa jamii imezipuuza mira na desturi kwa asilimia kubwa watu wamejikita zaidi na maisha kusaka fedha kiasi kwamba hata mtoto akidanganya juu ya jambo lolote mzazi hawana habari.
“Wazazi wamewatupia mzigo mkubwa walimu shuleni kiasi kwamba nao wanalemewa maana wanamajukumu yao, hivyo wazazi wabadilike.
“Wazazi washikamane ili kuwasaidia watoto kupata chakula shuleni ili kuwasaidia kuepuka vishawishi na mambo mengi wanayokubana nayo njiani. Hebu tujiulize mtoto wa wakike anatembea kwenda shule umbali Mrefu bila kula chochote, nyumbani pia anashinda njaa mpaka jion,i hivi hatuoni hali hii kuwa ni changamoto? wazazi tujitafakari,” amesema Nestory na kuongeza kuwa:
“Sisi shirika la Humuliza tumeweka malengo ya kuwafikia watoto 2,600 kila mwaka kwa zaidi ya miaka mitano sasa tukitoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto ambao wamekuwa wakipatwa na changamoto mbalimblia ikiwamo ukatili pamoja na mimba za utotoni,” amesema Nestory.
Aidha, Mkurugenzi amesa kuwa wanapokuwa wakitoa msaada wa kisaikolojia kwa watoto wanawaambia kuwa kunawazazi wengine wanapo wapa mahitaji ya shule mara moja huwa hawarudii tena kuwanunulia mahitaji sasa jambo la kujiuliza hivi hayo mahitaji huwa hayaishi hivyo wazazi wenzangu tujitathimini katika hili na tuchukue hatua.
Kwa upande, wake Meneja mradi, Lightness Mpunga, amesema kuwa asilimia kubwa watoto wapo kwenye mazingira hatarishi kuanzia shuleni na hata nyumbani.
“Napata shida Sana kurizungumzia hili kwani watoto wapo katika mazingira hatarishi maana ndani unamkuta mjomba, baba mdogo au babu wote hao ni shida katika malezi ya watoto jamii ibadilike mtoto wa mwenzio niwako na hili limekuwa tatizo kubwa sana watoto inakuwa ngumu kusema kuwa nimefanyiwa ukatili,” amesema Mpunga.
Mtoto amekuwa akiwindwa kila kona hivyo wazazi watenge muda wa kuongea na watoto kuwaweka wazi ili wajue nini kibaya kwao.
Mpunga amesema katika kuangalia ulinzi wa watoto wazazi wawe makini kwani kuna wakati unamkuta mzazi anawasha Tv na wanaangalia watoto kwa maana dada na kaka mwisho wa siku wanaweka picha za ngono na baada ya hapo wanafanya majaribio.
Kwa kipindi cha mwaka 2021 yameripotiwa matukio 74 yanayo husishwa na watoto ambao wamefanyiwa ukatili wa aina mbalimbali .
“Nitumie nafasi hii kuwaomba wazazi kuepuka kuwalaza chumba kimoja na wageni ili kuwalinda watoto maana dunia imebadilika sana ni bora mgeni alale chini lakini mtoto wako awe salama,” amesema Meneja huyo.