22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi washauriwa kusoma masomo ya usafiri wa Anga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanafunzi wa elimu ya juu, msingi na sekondari wameshauriwa kusoma masomo ya usafiri wa anga ili kupunguza ukosefu wa marubani na wahandisi katika sekta hiyo hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa usafiri wa anga kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Daniel Malanga wakati wa mdahalo juu ya umuhimu wa sekta ya anga katika maendeleo na ukuaji wa uchumi ulioandaliwa na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Malanga amesema taifa bado linakabiliwa na ukosefu wa marubani na mainjinia wa ndege, hivyo kama wanafunzi kuanzia ngazi ya msingi, sekondari watasoma  masomo ya sayansi na wanapofika elimu ya juu kuchukua yale yanayohusiana na usafiri wa anga upo uwezekano wa kupunguza tatizo hilo.

“Tupo nyuma kwa upande wa marubani na mainjinia wa ndege na hii inatokana na gharama na kuwepo kwa wanafunzi wachache wanaopenda masomo hayo ndio maana TCAA tunaendelea kuwahamasisha wanafunzi kusoma masomo ya usafiri wa anga ili nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha wa kuziendesha ndege zetu.

“Tunaziona juhudi za serikali za kuhakikisha kunakuwepo na vyuo vya kutosha vya kutoa elimu hiyo kikiwemo chuo cha NIT, hii itasaidia watu kusoma hapa nchini kwa gharama nafuu na kuzisaidia kampuni za ndege kupata wataalamu hapa hapa nchini kuliko hivi sasa ambapo ulazimika kuwatoa nje ya nchi kwa gharama kubwa,” amesema Malanga.

Mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Denis Mkocha.

Amesema sekta ya usafiri wa anga ni muhimu katika nchi yoyete ile duniani inayokuza uchumi wake hivyo ikiporeshwa na kuwa ya gharama ndogo, nafuu na ushindani mzuri faida kubwa itakuwepo.

Naye Meneja wa mtandao wa safari na usimamizi wa Mapato wa Shirika la Ndege Tanzania, Edward Nkwaki amesema kwa sasa shirika hilo lina ndege 12 ambapo aina ya Bombarded tano, Airbus8020 nne na ndege mbili kubwa.

Amesema ndege hizo zinahitaji marubani wa kuziendesha na mainjinia wa kuzifanyia matengenezo mbalimbali hivyo anawashauri wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya sayansi ili kuisaidia nchi kupata wataalamu wa kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Shirika la Ndege la Precision Air, Patrick Mwanri amesema wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha nchi inapata wataalamu wa kutosha katika sekta ya anga.

“Shirika letu tumekuwa tukiwasomesha wanafunzi wenye nia ya kusoma masomo ya sayansi na usafiri wa anga, na tumekuwa tukiwakata wateja wetu kiasi fulani cha fedha ili kuchagia programu hiyo,” amesemaMwanri.

Denis Mkocha mwanafunzi wa NIT amesema anatambua kuwa sekta ya anga ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi ndio maana aliamua kusoma masomo ya usafiri wa anga ili kuwa sehemu ya watu watakaoinua uchumi wa taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles