Mwandishi Wetu, Kibiti
Mkazi wa Kibiti mkoani Pwani, Yasin Yusuph Kingwande, amemshukuru mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kwa kumpatia shilingi milioni 30 alizoshinda kutoka kwenye mchezo wa kubashiri matokeo wa michezo mbalimbali duniani ya Bikosports, baada ya kupachika bao la ushindi katika mechi yao dhidi ya Azam FC.
Kingwande alibashiri mechi 12 na kuweka mtaji wa sh 500 na kumfanya aguse kilele cha ushindi kwa kubeti kuanzia mechi tatu na kuvuna hadi asilimia 100 kwa kupitia *149*89# wakitumia namba ya kampuni 101010 na wale wanaobeti kwa njia ya mtandao wa www.bikosports.co.tz.
Akizungumzia ushindi wake huo, Kingwande alisema Mayele ndiye aliyenusuru mkeka wake kwa kupachika bao la ushindi dhidi ya mpinzani wao Azam katika mchezo uliokuwa na msisimko wa aina yake akitupia bao katika mechi kubwa, akibeti kwa kutumia kampuni ya bikosports.
“Huwa naweka mkeka mara kwa mara kwa kupitia kampuni ya bikosports ambayo kwangu naona ni rahisi sana kubeti nao, nikiwa na shauku kubwa ya kuvuna fedha jambo ambalo limefanikiwa kwa kupitia matokeo mazuri ya mechi yangu ya mwisho kati ya Yanga na Azam FC.
“Watanzania wote hususan wale wanaopenda kubeti nawaomba watumie kampuni ya Bikosports kwa sababu hawana longolongo katika uendeshaji wao na huwa na bonansi nzuri kuliko kampuni zote zinazojua mimi,” alisema Kingwande.
Bikosports ni mchezo unaochezwa na Watanzania wote hususan wale wenye ndoto za kukuza uchumi wao ambapo kwa kupitia simu ya mkononi *149*89# au www.bikosports.co.tz wanaweza kucheza na kushinda fedha nyingi kama ilivyokuwa kwa Kingwande.