26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yamnasa aliyevunja madirisha ya shule Moro…

Na Ashura Kazinja, Morogoro.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Hussein Chidaka (53) mkazi wa kibedya kwa kosa la kuvunja madirisha 12 ya vioo kwenye madarasa sita yaliyojengwa kwa fedha ya Uviko-19 katika shule ya sekondari Kibedya wilayani Gairo mkoani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu Aprili 11, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Fortunatus Musilimu, amesema baada ya mahojiano mtuhumiwa alidai sababu ya kufanya hivyo ni wivu mapenzi.

Amesema tukio hilo limetokea Aprili 6, 2022 saa sita na nusu usiku na kuripotiwa katika kituo cha polisi Gairo saa mbili asubuhi siku hiyo na kwamba baada ya taarifa hiyo walimtafuta mwalifu na kufanikiwa kumkamata mwalifu huyo.

“Tulimfanyia mahojiano na katika mahojiano hayo alikii kuhusika katika tukio hilo la kuvunja madirisha kwa kutumia nyundo na katika mikono yake tulimkuta na majeraha kwamba wakati anavunja yale madirisha anapiga vioo vipande vya kioo vilimkata katika mikono yake, huo ni ushahidi wa kwanza, na tumechukua damu yake tuliyoikuta kwenye vioo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu kwa maana ya kuangalia vinasaba,” amesema Kamanda Muslim.

Amesema baada ya kumuhoji zaidi alisema amefanya tukio hilo kutokana na wivu wa mapenzi, baada ya kumfumania mlinzi washule hiyo akiwa na mke wake na akaamua kumuacha, lakini kilichomuumiza zaidi ni kitendo cha mlinzi huyo kumchukua na kuishi nae kama mke wake, kitendo kilicho mkera na kujenga chuki kati yao, na ndipo alimoamua kuondoka usiku huo na kwend katika eneo la shule na hakumkuta mlinzi na kuamua kuvunja vioo vya madirisha ili kulipa kisasi.

“Hivyo amesema aliamua kufanya hivyo ili kwamba watakapokuta vioo vimevunjwa na mlinzi hayupo basi aweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, lakini kwa sababu jeshi la polisi lina mkono mrefu tumeweza kufatilia kwa karibu zaidi na kuweza kumtia mbaroni na upelelezi umekamilika tunaandaa taratibu za kumfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria,” amefafanua kamanda Muslim.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia watu 25 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kukutwa na nyara za Serikali, kumiliki kiwanda cha kutengeneza vinywaji bandia aina ya Smart GIN.

Kamanda Muslim amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika doria, msako na operesheni za kuzuia uhalifu.

Ameyataja makosa mengine kuwa ni vipande 18 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogram 61, stika zenye nembo ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) pamoja na vinywaji bandia aina ya smart GIN.

Aidha, Kamanda Musilimu amesema wamefanikiwa kuwakata wazalishaji na wasambazaji wa vinywaji bandia ambao amewataja majina kuwa ni Sengo Manyulizi, Richard Lipendele na Dennis Keula kwa kumiliki kiwanda cha kutengeneza vinywaji bandia aina ya smart GIN na rivella. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles