21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Makala| Njombe yachechemea chanjo ya Uviko-19

*Mkuu wa Mkoa ataka juhudi za makusudi kuchukuliwa

*Wataalam wazidi kutoa elimu…

Na Elizabeth Kilindi, Njombe.

“Chanjo ya corona wanatakiwa wachanje wazee na watu ambao wanamagonjwa sugu, mimi kwa umri huu siwezi kuchanja hivi kwani bado ipo?,” anasema Marcus Mlowe Kijana mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa mtaa wa kambarage mjini Njombe alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa makala hii juu ya jamii mkoani humo kukosa muamko kuhusu kuchanja chanjo ya Uviko-19.

Kwa uelewa wake mwenyewe, Mlowe anaamini kuwa chanjo hiyo inapaswa kutolewa kwa watu wenye magonjwa sugu kama wenye maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI(VVU), Presha, Saratani na Kisukari.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, akipata chanjo ya Covid-19, Ikulu jijini Dar es Salaam, Julai 28, 2021. Picha na Maktaba.

Anasema kwanza yeye hawezi kupata ugonjwa wa Uviko-19 kwa sababu bado ni kijana na hana wagonjwa sugu.

Hata hivyo, uelewa wa Mlowe unatokana na kukosa elimu sahihi juu ya chanjo hii kwamba inaweza kumkinga kutokupata ugonjwa wa Uviko-19.

Had watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo watu kadhaa kutoka nchini kwetu wakiwemo vijana na wazee.

Katika swala la uhamasishaji wa chanjo ya Uviko-19 mkoa wa Njombe unatajwa kusuasua katika swala la uchanjaji na hii inatokana na kukosekana kwa elimu sahihi.

Gaston Kilamlya mkazi wa Njombe anasema mwanzo hata yeye hakua na elimu sahihi juu ya chanjo ya Uviko-19, hivyo alidhani chanjo inaweza kumletea madhara hata kusababisha kifo.

Kilamya anasema kuwa mara baada ya kupata elimu sehemu mbalimbali aliamini na kwenda kuchanja.

“Chanjo ya Uviko 19 haina madhara mimi mwenyewe nimechanja ni imani potofu tu ambayo imetengenezwa kwa watu ili kukufisha juhudi za serikali katika kuhakikisha afya njema kwa wananchi wake,’’anasema Kilamlya.

Anaongeza kuwa: “Ni upotoshaji ambao upo mtaani mbona mimi nimechanja niko salama, nafanya kazi zangu nadhani elimu iendeleee kutolewa,” anasema Kilamlya.

Naye Muuguzi Furaha Ngota kutoka zahanati ya Kitulila anasema jamii inabadilika taratibu hasa maeneo ya vijijini ila changamoto ipo mijini.

“Vijijini wakipata elimu ya kutosha tutaongeza idadi ya wachanjaji vile vile mijini ambako nako mwamko mdogo kutokana na maudhi madogomadogo yaliyotokea awali katika chanjo ya J&J,”anasema Ngota.

Wananchi walio wengi wameacha kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 kwa sababu wanaamini ugonjwa huo haupo tena.

Hata hivyo, jitihada za elimu pamoja na tahadhari kama matumizi ya vitakasa mikono, kunawa maji tiririka na sabuni sambamba na uvaaji barakoa kwa usahihi.

“Awali, wakati ugonjwa huu unaripotiwa mwishoni miaka 2019 majumbani, sehemu za starehe, usafiri wa umma walikua wakizingatia maelekezo ya wizara ya Afya ambapo ni tofauti na hivi sasa.

“Jamii inapaswa kifahamu chanjo ya Uviko-19 haina madhara yoyote kwa binadamu hivyo ni vyema wakapate chanjo hiyo ili kuwa salama kwa sababu ugonjwa bado upo,” anasema Ngota.

TAKWIMU

Tangu zoezi la uhamasishaji chanjo ya Uviko-19 lianze kwa upande wa Halmashauri ya mji Njombe wananchi 8,000 sawa na asilimia 9 wamefikiwa huku lengo likiwa nikufikia asilimia 60.

Kwa upande wa mkoa wa Njombe wananchi wapatao 35,000 sawa na asilimia 10 ndio wamepata chanjo ya Uviko-19, huku lengo likiwa ni kuchanja asilimia 70 wenye umri kuanzia umri wa miaka 18.

CHANJO YA UVIKO 19 YAWA AGENDA KIMKOA.

Akizungumza katika mikutano mbalimbali mkoani hapa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba anasema bado kunahitajika msukumo wa uhamasishaji wa chanjo ya Uviko-19.

“Chanjo ni hiyari, lakini sisi ambao tumepewa dhamana ya kuangali hali za watu ni lazima tuhamasishe watu wakapate chanjo. Kwa hiyo nitatamani sana tukahamasishane na tubadilishe tutoke huku chini tupande na sisi tuonekane watu wamepata chanjo.

“Mimi mwanzoni pia nilikua muoga muoga hivi mara mtu kachanja kaweka Shilingi imenasa kwamba ukiweka inakua kama sumaku na mwengine anasema hivi kwa hiyo maneno maneno yalikua mengi hasa sisi tunaoshinda kwenye mitandao na sisi vijana na mambo yamekwisha kwa hiyo nikataka kujifunza nikajua kumbe ni maneno nikaenda kupata chanjo yangu hadi hivi sasa nadunda niko safi,” anasema Kindamba.

Mkuu huyo wa mkoa anasema watu wamejazwa hofu juu ya chanjo ya Uviko 19 na hivyo inapaswa kuondolewa.

“Mara mia ugonjwa kama Uviko-19 ukukute ukiwa tayari unachanjo kuliko ambaye hajachanja, lakini pia uwezo wa kupoteza maisha ni mkubwa kwa mtu ambaye hajachanja ukilinganisha na mtu ambaye amechanja kwa hiyo twendeni tukahamasishane na tuanze na hapa kwetu, tuhamasishe watumishi wote ofisini kwetu tukiweza kuchanja tutakua mabalozi wazuri wa kuisemea chanjo kwa wananchi wa kawaida,” anasema Kindamba.

Anasema kuwa: “Sasa kama sisi hapa wenyewe tutakua na mashaka itakua ngumu kuwashawishi raia huko mtaani kwa hiyo nitaomba nipriti cheti changu nibandike hapa ili wasije wakasema jamaa anatupiga changa la macho kitakaa humu ili kila mtu aone na bado nadunda natekeleza majukumu yangu,” anasema Kindamba.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji Njombe, Isaya Mwasubila, anasema wananchi wengi walidanganywa na taarifa za mitandaoni juu ya chanjo ya Uviko 19 kwamba inamadhara.

“Wengi walidanganywa na taarifa potofu za mitandao ambayo ulikua sasa ni changamoto kubwa lakini pia swala la elimu wananchi bado hawakua na elimu sawa sawa lakini hivi wameanza kupata muamko,” anasema.

Anasema kuwa wananchi wanapaswa kuondokana pia na imani potofu kwamba wazee tu na wenye magonjwa sugu ndio wanaweza kupata ugonjwa wa Uviko 19.

“Makundi haya tulisema tu kwa sababu tunajua kinga zao zimepungua wanakua na wakati mgumu na ni rahisi wao kuugua ugonjwa wa Uviko 19 ukilinganisha na wale ambao ni wazima na aina maana kwamba wale ambao hawana magonjwa sugu na wazee kwamba hawatougua Uviko 19,” anasema.

Anaongeza kuwa: “Tumepoteza watu wengine ambao ni vijana kabisa ambao wala hawakua na magonjwa sugu,’’ anasema.

Mwasubila anatoa rai kwa wananchi kuachana na dhana kwamba wazee au watu wenye magonjwa sugu ndio wanapaswa kuchanja bali ilikua ni kipaumbele kwa sababu kinga zinakua zimepungua.

Anasema walijiwekea malengo kwamba angalau wafikie asilimia 60 lakini kutokana na changamoto hiyo wamefikia asilimia tisa pekee.

“Na sasa hivi tunaongea hivi tumefikia asilimia tisa tu hii ni changamoto kubwa ambapo Sasa hivi kuna kampeni ambayo ni ya mkoba ili kutoa elimu kutokana na wanaNjombe kudanganywa na mitandao,” anasema Mwasubila.

KUHUSU KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME.

Erasto Mgaya anasema kuwa mwanzo hata yeye mwanzo aliamini kuwa chanjo ya Uviko 19 inapunguza nguvu za kiume: ’’Jamani wanaNjombe wenzangu chanjo hii haina uhusiano wowote na swala la Nguvu za kiume mimi nimechanja J&J wala sikuona tofauti wala malalamiko kutoka kwa mke wangu,tuache visingizio twendeni tukachanje ili kulinda afya zetu,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles