29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kupima upya eneo la Nanyala kuondoa mgogoro

Na Denis Sinkonde, Songwe

Serikali mkoani Songwe imesema ina mpango wa kuligawa eneo la zaidi ya ekari 1,800 lenye hati namba 31 lililopo Kijiji cha Nanyala ambalo kwa muda mrefu limekuwa na mgogoro kati ya kiwanda cha saruji cha Mbeya, wananchi wa Kijiji cha Nanyala na wadau wengine ambao wanafanya shughuli za uchimbaji madini katika kijiji hicho.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema hayo Aprili 8, 2022 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Nanyala, Mbeya Cement na wadau wanaofanya shughuli za uchimbaji katika Kijiji hicho kata ya Nanyala wilayani Mbozi mkoani humo.

Mgumba amesema timu ya wataalamu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan itapita kubaini maeneo yanayofaa kwa Kiwanda cha Mbeya Cement, kwa Kilimo, madini ya chokaa, marble na eneo la wananchi ili kila mtu abaki na eneo ambalo linafaa kwake kwa shughuli za kiuchumi.

Mgumba amesema kuna mgogoro kwa sababu serikali ilitoa hati ya miaka 99 ya kiwanja namba 31 kwa kiwanda cha Mbeya Cement, wakati wapo wananchi wanaomiliki kisheria na wana hati za kimila, kuna wengine wameachiwa na babu zao pia kuna wadau wanafanya shughuli za uchimbaji wa madini na wamepewa leseni halali na serikali ya Tanzania.

“Kiwanda cha Mbeya Cement kimeondoa kesi Mahakamani baada ya kuona hakuna masilahi ya kuendelea na kesi Mahakamani wakati wana uwezo wa kumaliza mgogoro huo kwa pamoja kati ya Mbeya Cement, wananchi wa Nanyala, wadau wanaofanya shughuli za uchimbaji na Serikali,” amesema Mgumba.

Diwani wa Kata ya Nanyala, George Musyani ameishukuru serikali kuja na mpango wa kupima upya ardhi kwani ndani ya ekari 1,800 ambazo Mbeya Cement wanadai ni za kwao na wananchi wa Nanyala wanalitegemea kiuchumi kwani wana mashamba yao, migodi na baadhi ya vitongoji vipo umo kama cha Majimoto, Iwanga, Udinde, Malema ambayo kuna miundombinu ya huduma za jamii.

Naye Julius Mwashilindi mwananchi wa Kijiji cha Nanyala alisema kitendo cha Mbeya Cement kuamua kumiliki ardhi bila ya kuwa na mkutano wa hadhara na kijiji ndio chanzo kikubwa cha mgogoro.

Mkazi wa Nanyala, Aneth Gambi alisema ardhi ya Nanyala ni mali yao ambayo vizazi kwa vizazi vimeishi pale na wameiomba serikali kuwasidia kutatua mgogoro huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles