25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Japani yafadhili ujenzi wa bweni Sekondari ya Itona wilayani Mufindi

Na Raymond Minja, Mtanzania Digital

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imetiliana saini na Serikali ya Japani kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini kufadhili ujenzi wa bweni la Wasichana katika shule ya sekondari Irina iliyopo kata ya Ifwagi wilayani Mufindi.

Kandarasi hiyo ya kujenga bweni la wasichana katika Shule hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia Machi 8, 2022 kwa gharama ya Dola 101,363 sawa na Sh milioni 231.48.

Bweni hilo ambalo ni muhimu uhimu katika Jitihada za Kuistawisha Elimu ya Mtoto wa Kike Katika Halmashauri ya hiyo Litakuwa na uwezo wa Kuchukua Wanafunzi themanini (80) kwa wakati Mmoja likiwa na Vitanda Sanjari na Matanki ya Kuhifadhia Maji kwa Matumizi ya Wanafunzihao .

Hafla yhiyo imetekelezwa katika ofisi za Ubalozi huo zilizopo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji, Zaina Mlawa pamoja na Balozi wa Japani nchini, Goto Shinichi.

Wengine walioshuhudia utiaji saini huo ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mwenyekiti wa Halmashauri, Afisa Elimu Sekondari, Mwanasheria wa Halmashauri, Mhandisi wa Ujenzi, Mkuu wa Shule ya Itona na Maafisa wa Ubalozi wa Japani.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri ya Mufindi ameushukuru uongozi wa ubalozi wa Japan kwa kuweza kushirikiana na wilaya hiyo katika kufadhili ujenzi wa bweni hiyo.

Mtambule amesema kuwa bweni hilo ni muhimu kwa ustawi wa elimu kwani itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zikiiwemo za wanafunzi kutembea umbali mrefu na pia kuwaepusha wanafunzi hao kupata ujauzito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles