25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TAEC: Hakuna tozo kwa wafanyabiashara wadogo

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imekutana na wadau mbalimbali kupitia mapendekezo ya marekebisho na maboresho ya kanuni za tozo ambapo imesema wafanyabiashara wadogo wadogo hawatatozwa tozo yoyote katika ufanyaji biashara zao.

Akizungumza Februari 15, 2022 jijini Dodoma katika kikao cha pili cha kupitia mapendekezo na marekebisho ya ada na tozo, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Alexander Mtawa amesema kikao hicho kitasaidia kuleta maboresho ya kanuni za nguvu za atomiki nchini.

Dk. Mtawa ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema kupitia mapendekezo hayo wafanyabiashara wadogo wadogo hawatatozwa tozo yoyote katika ufanyaji biashara wao.

“Tunahakikisha biashara za vyakula zinakuwa na ubora na kwa sasa hatuna madhara yoyote ambayo yamejitokeza kutokana na mionzi,” amesema amesema Dk.Mtawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala amebainisha malengo ya kikao hicho ni pamoja kujadili namna ya  kuwalinda wananchi wasidhurike na madhara yatokanayo na mionzi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya usafirishaji wa bidhaa, Tanzania Exporters Association (TANEXA), Peter Lanya amesema kupitia maboresho hayo watafaidika na hivyo biashara kufanyika kiurahishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles