23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

NMB kuwakomboa Wamachinga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KWA mara nyingine Benki ya NMB imeonyesha ni benki inayojali watu wa hali zote kiuchumi na kijamii, imeungana na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) katika kuhakikisha wafanyabiashara wenye mitaji midogo wanakua kibiashara.

Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania(SHIUMA), Ernest Masanja wakibadirishana nyarakka baada ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Shirikisho la Umaoja wa Machinga Tanzania na  Benki ya NMB wakati wa hafla iliyofanyika Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Huduma wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli na kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na  Makundi Maalum, Juma Samuel.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ghafla ya kutiliana saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara NMB, Filbert Mponzi alisema benki hiyo ni kinara wa kushirikiana na wajasiriamali wa viwango vyote nchini.

“Tangu zamani ilipoanzishwa benki hii ilichagua kuwa na watu wa hali zote kuanzia wa juu hadi chini, kama mtakumbuka ndiyo maana ilikuwa ikiitwa benki ya makabwela. Matawi yetu yaetapakaa nchi nzima, tuna mashine za ATM na mawakala ambao watawafikia wateja wetu popote walipo,” alisema Mponzi.

Alibainisha kuwa mbali ya kutoa mikopo na mafunzo ya biashara, NMB kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Reliance watatoa huduma ya bima itakayolinda biashara za wamachinga dhidi ya majanga kama moto, ajali na mafuriko.

“Bima hiyo itaanzia Sh10,000 kwa mwaka ambapo mnufaika atapata hadi Sh 500,000. Lakini pia kua bima ya Sh 60,000 kwa mwaka ambapo mnufaika atapata hadi Sh Milioni 10 pale atakapopatwa na majanga yaliyoainishwa,” alisema Mponzi.

Aidha, Mponzi alisisitiza kuwa NMB inathamini juhudi za Wajasiriamali Wadogo Wadogo (SME’s) na kwa kuonyesha hilo imejikita zaidi katka kuhakikisha shughuli zao zinakua nchini na ndio maana imekuwa ikitoa mchango mkubwa kuwezesha sekta hiyo muhimu kibiashara nchini.

Mponzi alifafanua kuwa: “Kikubwa tumekubaliana kushirikiana kwenye maeneo ya kuongeza ujuzi wamachinga, mitaji na uwekezaji, uendelezaji wa biashara na upatikanaji wa fursa, taarifa sahihi za kibiashara, masoko, sera na maendeleo kwa wamachinga.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA), Ernest Masanja alisema benki ya NMB imewasaidia kwa kiasi kikubwa katika masuala mbalimbali ikiwemo mitaji na fursa za kukua kibiashara kwa miaka mingi.

“Hiyo, makualiano haya yanadhhirisha sasa ni rasmi hawa ni baba zetu, wameamua kutushka mkono baada ya kukumbwa na majanga mengi kama kuunguliwa na moto bishara zetu na kupotez amitaji. Rasmi sasa machinga hawatateseka nchini kwa kuwa tunatembea na NMB ambayo inajali watu wa chini.

“Naweza kusema wanyonge wote leo (jana) wamekombolewa kupitia makubaliano haya. Wamachinga tumeteseka kwa muda mrefu hatimaye mkombozi wetu amejitokeza. Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, hakika huu ni mwanzo mpya na amethibitisha kuwa wanawake wanaweza,” amesema.

Mkurugenzi Msaidizi kutokaWizara ya Maendeleo ya JamiiJinsia,Wanawake na Makundi Maluum, Juma Samwel alisema anaishukuru benki ya NMB na SHIUMA kwa makubaliano hayo ya kihistoria ya miaka mitano kwa kuwa wizara inatambua kupitia makubaliano hayo wmachinga wataendelezwa kiuchumi na kuongeza fursa za kibiashara. Lakini pia alibainisha kuwa wamachinga wote nchini watakuwa na ujuzi sawa kupitia mafunzo watakayopewa.

Naye Mwenyekiti wa SHIUMA Mkoa wa Arusha, Amina Njoka alisema: “NMB ni benki yangu tangu zamani, pia mkoani Arusha wamachinga wote tumefungua akaunti za NMBna Saccoss yetu inaweka fedha NMB. Niwakumbushe tu kuwa kundi hili la wamachinga ni kubwa, popote tulipo tunawategemea, msituache,”.

Itakumbukwa tangu mwaka 2000 benki ya NMB imekuwa ikitoa mikopo midogo kuanzia Sh 500,000 hadi Sh mililioni 5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles