28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vibarua wazuia msafara wa Waziri Mkuu

majiwa kasimuNa Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

VIBARUA wa Kampuni ya Tarmal iliyoko Mabibo, Dar es Salaam, wamezuia msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili asikilize malalamiko yao.

Malalamiko hayo ni ya kutokuwa na mikataba ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10 pamoja kutowekewa fedha zao kwenye mfuko wa Pensheni wa PPF.

Kampuni hiyo ni wakala wa Kampuni ya PSI inayohifadhi na kusambaza vifaa vya uzazi wa mpango.

Baada ya kusimamisha msafara huo, Mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Amin Athuman alimweleza waziri mkuu kuwa mwajiri wao anashindwa kuwalipa stahiki zao   wanapoacha au kusimamishwa kazi jambo ambalo limewatia woga na kushindwa kudai haki zao.

“Tunakuomba Waziri Mkuu utusaidie, tunanyanyasika sana kwenye kampuni hii lakini hatuna pa kukimbilia, ndiyo maana tulipoona msafara wako tuliamua kukusimamisha  kuwasilisha malalamiko yetu.

“Licha ya kuwapo   matatizo lukuki lakini pia mpaka sasa hakuna mkataba wa kudumu, jambo ambalo limetufanya tuwe vibarua kwa zaidi ya miaka 10 sasa,”alisema Athuman.

Majaliwa aliwaambia wafanyakazi hao kuwa  hawezi kulifumbia macho suala hilo kwa sababu linachangia kuongezeka   vitendo vya unyanyasaji kazini.

Alimwagiza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama  na Mikurugenzi wa PPF kufika kwenye ofisi hizo kusikiliza kero za wafanyakazi hao na kuchukua hatua stahiki.

Majaliwa alikumbana na kadhia hiyo ya wafanyakazi wakati akitoka kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 10 ambavyo vilitolewa na Umoja wa kampuni zinazotengeneza vinywaji baridi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles