32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaleta nongwa sasa

kikosi cha yanga 2016*Eti yajitoa ushindani na Simba wa mchangani

ADAM MKWEPU NA SUZANA MAKORONGO, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga umetangaza kujitoa kwenye ushindani wa kimchezo dhidi ya mahasimu wao, Simba, katika Ligi Kuu Tanzania Bara, badala yake watabaki kuwa watani kawaida.

Yanga imefikia hatua hiyo, baada ya kuwafunga mahasimu wao hao mabao 2-0 kwa mara ya pili mfululizo, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa  Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Awali walifanya hivyo Septemba 26, mwaka jana, katika mzunguko wa kwanza.

Ushindi wa Yanga umeifanya timu hiyo kurejea kileleni ikiwa na pointi 46, huku watani wao wa jadi, Simba, ikiwa nafasi ya tatu wakiwa  na pointi 45 sawa na timu ya Azam, ambayo wametofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Msemaji wa klabu hiyo, Jerry Muro, alisema  hatua hiyo inatokana na rekodi ya kuwafunga watani hao  mara nyingi zaidi na kuongeza  kuwa jambo hilo  limeonekana kuondoa ladha ya ushindani.

“Hatujakurupuka, tumekaa tumetafakari, tumecheza mara  92  dhidi ya Simba, tumefanikiwa kuwafunga mara 35, wao wakipata  ushindi mara 25 na sare 32, tumewaacha kwa pengo la michezo 10.

“Kuanzia leo Simba hawatakuwa wapinzani wetu tena, tutabaki kutaniani kwenye vijiwe vya kahawa kutokana na kuwapo kwa historia ndani yetu, lakini si ushindani wa soka, shukrani ziwaendee benchi la ufundi na kocha Hans van Pluijm,” alisema Muro.

Murro alisisitiza kuwa baada ya ushindi huo wanajipanga ili kufanya vizuri kwenye michuano ya FA, michezo ya Ligi Kuu iliyobakia na Klabu Bingwa Afrika.

“Tumeanza leo mazoezi katika uwanja wa Polisi Kurasini  ili kujiandaa na mchezo wa FA, baada ya hapo tutakuwa na mchezo wa marudiano na timu ya Cercle de Joachim  ya nchini Mauritius ,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles