26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Walemavu walia na vyama vya siasa

stellaNA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

VYAMA vya siasa vimeombwa kuweka misingi imara ya kuwainua watu wenye ulemavu na kuacha kuwawekea vikwazo kwa kuhofia kushindwa katika uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), kuhusu namna vyombo vya habari vilivyominya sauti za wanawake.

Semina hiyo iliwahusisha waandishi wa habari pamoja na watu wenye ulemavu waliogombea uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Stella Jailos ambaye ni mlemavu wa macho, aligombea Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dodoma.

Alisema walikumbana na changamaoto mbalimbali katika uchaguzi huo ikiwamo kutokuaminiwa na vyama kama kweli wanaweza kuleta ushindi.

Aidha Stella alisema alishuhudia unyanyapaa wa wazi hata katika majukwaa ili kunadi sera zao kwani waliambiwa muda umekwisha jambo ambalo liliwafanya wajisikie kutengwa katika vyama.

“Kwa upande wetu sisi walemavu nafikiri hata ndani ya vyama vyetu bado hawana uhakika kama sisi tunaweza kuuzika au laa…kuna unyanyapaa wa wazi hawatuamini kama tunaweza kuleta ushindi katika vyama vyao,”alisema Stella.

Kwa upande wake, Said Ndonge ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino), alisema watu wenye ulemavu hawaonekani kama wana uwezo wa kuchagua au kuchaguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles