25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Nissan Tanzania watambulisha gari jipya Magnite

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Magari ya Nissan Tanzania imetambulisha gari jipya aina ya Magnite ambalo limebuniwa kukidhi mazingira ya hapa nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Nissan Tanzania, Christopher Henning, akizungumza wakati wa uzinduzi wa gari jipya aina ya Magnite. Katikati ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Alfred Minja na Meneja Ufundi, Sameer Amir.

Akizungumza leo Novemba 3, wakati wa kutambulisha gari hilo uliofanyika katika ofisi za kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Nissan Tanzania, Christopher Henning, amesema Magnite ni imara kwani limebuniwa kwa ubora wa hali ya juu.

“Ni gari ambalo limeongezwa nguvu zaidi kulinganisha na magari mengine ili kila mtu aweze kulitumia,” amesema Henning.

Naye Meneja Masoko wa Nissan Tanzania, Alfred Minja, amesema gari hilo ambalo ni toleo la mwaka 2020 linauzwa Dola za Marekani 25,000 sawa na Sh milioni 59.5.

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya biashara hapa nchini katika sekta ya usafirishaji tangu mwaka 2015 na mpaka sasa imeshatambulisha magari mbalimbali ambayo yanatamba sokoni.

Kwa upande wake Meneja Ufundi wa kampuni hiyo, Sameer Amir, amesema gari hilo linatumia lita moja ya petroli kwa kilomita 17 hadi 18 na kwamba baada ya miaka miwili hufanyiwa ‘service’ bure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles