24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

GIZ yamwaga vifaa tiba hospitali za Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh 747 kwa hospitali na vituo vya afya vya Mkoa wa Tanga.

Vifaa hivyo ni pamoja na Mashine ya joto, Oksijeni ikiwa ni teknolojia ambayo haihitaji mtungi na ina uwezo wa kuhudumia hadi watoto wawili kwa wakati mmoja, friji la kuhifadhia damu kwa ajili ya mama na mtoto na vingine vingi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tangq, Pili Mnyema akipokea msaada wa vifaatiba vyenye thamani ya Sh milioni 747 kutoka kwa Meneja Mradi wa Afya wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), Erick Msoffe.

Akipokea vifaa hivyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema amesema vifaa hivyo wamepatiwa na GIZ kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wanaboresha huduma ya afya hususani huduma ya mama na mtoto ambapo vinaenda kusaidia watoto wanaokumbana na changamoto ya kuzaliwa kabla umri haujatimia.

“Kama tunavyofahamu Mkoa wa Tanga kuna wilaya nane na hizi wilaya ziko mbalimbali kwa hiyo mama anapojifungua mtoto kabla siku hazijatimia na yuko mbali kutoka katika hospitali ambazo ziko mbali na mkoa inakuwa ni changamoto na wakati mwingine watoto hupoteza maisha,” amesema.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Afya wa GIZ, Erick Msoffe, amesema lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha huduma ya mama na mtoto hususani wale wanaozaliwa kabla ya wakati.

“Ushirikiano wetu ni wa muda mrefu vifaa hivi vimekuja lakini tulishaanza kufanya kazi katika vituo hivi vya mkoa kwa ushirikiano na Katibu Tawala wa Mkoa kwa kuanza na mafunzo kwa watumishi jinsi ya kuwashughulikia na kuwahudumia kinamama wajawazito na watoto wachanga ambao wanaugua baada ya kuzaliwa.

“Ili kutoa huduma na kutumia vifaa hivyo kwa ufasaha tumewapeleka manesi kozi ya usingizi ya mwaka mmoja na tunaamini sasa hivi serikali ina nia kubwa ya kuhakikisha kuwa huduma za mama na mtoto zinatolewa kuanzia vituo vya chini kwa hiyo manesi hao watakwenda kusaidia watoto hao wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo sana wakati mwingine inakuwa vigumu kuwachukua katika vituo na kuwaleta katika hospitali ya mkoa au wilaya.

“Kwa hiyo mafunzo haya yatasaidia kwamba basi mtoto yule pale alipo walau aweze kupata huduma ya afya kwa hiyo tunaomba vifaa hivi vikasaidie huduma hizi,” amesema Msoffe.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jonathan Budenu, amesema vifaa hivi vitagawanywa katika vituo na Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Hospitali ya Rufaa Bombo, Kituo cha Afya Ngamiani, Maramba, Hospitali ya Wilaya Lushoto, Korogwe, Magunga, Handeni Mji na Kituo cha Afya Mkata.

Amesema kila kituo kimepata vifaa kama hivyo kwa hiyo kuna uhakika ile changamoto ambayo inatokana na kukosekana na huduma hizo zitapatikana kwa kwa ukaribu na wanaamini kutokana na mafunzo mbalimbali yaliyofanyika na upatikanaji wa vitendea kazi katika hospitali na vituo vya afya vitaenda kuokoa watoto hao.

“Hapa tumepata mashine ya kumsaidia mtoto kupumua akiwa katika kusafirishwa au anapozaliwa akashindwa kupumua, vifaa vya kumsaidia mtoto kuwekwa katika mazingira rafiki kama amezaliwa kabla ya muda. Baadhi ya vifaa vimeshaanza kufungwa katika hospitali zetu, wilaya, vituo vya afya na hospitali ya mkoa.

“Kutokana na tulichojifunza hata mtoto akizaliwa na nusu kilo na kuendelea ukiwa na vifaa hivi unaweza kumtunza na akaishi. Tunaahidi kuvitunza na tutaweka bajeti kwa ajili ya kuviweka vidunu kwa muda mrefu kusaidia wananchi kupata huduma stahiki,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles