27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Zabibu Zena atambulisha ‘Niongoze’

Idaho, Marekani

MWIMBAJI anayekuja kwa kazi kwenye muziki wa Injili kutoka Idaho nchini Marekani, Zabibu Zena amewaomba wapenzi wa muziki huo kuipokea video ya wimbo wake mpya, Niongoze.

Akizungumza na mtanzania Digital, Zabibu Zena amesema huo ni wimbo wa kuonyesha uzuri wa mwanadamu kumpa nafasi Mungu aongoze maisha ya mtu binafsi.

“Nashukuru mapokezi yamekuwa makubwa, naamini wimbo huu utawabariki wengi sana kutokana na ujumbe wake, naomba mashabiki na wapenzi wa muziki wa Injili waingie kwenye chaneli yangu ya YouTube kutazama video hii,” amesema Zabibu ambaye aliwahi kutamba na wimbo Vibaya aliomshirikisha Boni Mwaitege.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles