ASILIMIA 33 ya watoto nchini wanakabiliwa na upungufu wa vitamini A kutokana na kukosa lishe bora kwa mujibu wa kanuni za afya.
Wanawake walioathirika ni asilimia 37.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki mjini Morogoro na Mratibu wa PANITA Tanzania, Jane Msagati.
Alisema jamii haina budi kuhakikisha inatoa kipaumbele kwa watoto kupata lishe bora.
Alisema ikiwa hatua muhimu zitazingatiwa ikiwamo watoto kupata lishe bora kuanzia ujauzito wa mama hadi mtoto anazaliwa, humjenga akili na mwili kwa kuwa na uwezo wa kufanya viziri katika masomo yake.
“Zaidi ya asilimia 59 ya watoto chini ya miaka tano wana upungufu wa damu (aneamia) na karibu asilimia ya kina mama wana upungufu wa damu. Ikiwa lishe bora atapewa mtoto katika ziku 1000 za mwanzo itasaidia kumjenga mwili na akili.
“Kama atapata virutubisho ambavyo ni viini vidogo vinavyotengeza chakula ambavyo ni protini, wanga, vitamini, madini , nyuzi nyuzi na maji na kukosekana kwa lishe bora husababisha utapiamlo.
“Na hivi karibuni kuna utapiamlo unaotokana na unene kupita kiasi na upungufu wa virutubishi vya vitamini na madini ndiyo unaoathiri zaidi sehemu kubwa ya jamii,” alisema Jane.
Alisema utapiamlo huwaathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wsa umri wa uzazi.
“Mwili wa binadamu hauna uwezo wa kutengeneza virutubishi. Ukosefu wa virutubishi hivi mwilini husababisha njaa iliyofichika (hidden hunger) na huchangia kwa kiwango kikubwa katika kusababisha magonjwa na vifo hususan kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na kina mama walio katika umri wa kuzaa.
“Vitamini na madini hufanya kazi mbalimbali mwilini kama vile kusaidia kuupatia mwili nguvu na joto, kuujenga na kuulinda dhidi ya magonjwa mbaliambali,” alisema