31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto waathirika kwa kukosa vitamin A

vitamin ANa Mwandishi Wetu, Morogoro

ASILIMIA 33 ya watoto nchini wanakabiliwa na upungufu wa vitamini A kutokana na kukosa lishe bora kwa mujibu wa kanuni za afya.

Wanawake walioathirika ni asilimia 37.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki mjini Morogoro na Mratibu wa PANITA Tanzania, Jane Msagati.

Alisema jamii haina budi kuhakikisha inatoa kipaumbele kwa watoto kupata lishe bora.

Alisema ikiwa hatua muhimu zitazingatiwa ikiwamo watoto kupata lishe bora kuanzia ujauzito wa mama hadi mtoto anazaliwa, humjenga  akili na  mwili kwa kuwa na uwezo wa kufanya viziri katika masomo yake.

“Zaidi ya asilimia 59 ya watoto chini ya miaka tano wana upungufu wa damu (aneamia) na karibu asilimia ya  kina mama wana upungufu wa damu. Ikiwa   lishe bora atapewa mtoto katika ziku 1000 za mwanzo itasaidia kumjenga  mwili na  akili.

“Kama atapata virutubisho ambavyo ni viini vidogo  vinavyotengeza chakula ambavyo ni protini, wanga, vitamini, madini , nyuzi nyuzi na maji na kukosekana kwa lishe bora husababisha utapiamlo.

“Na hivi karibuni kuna utapiamlo unaotokana na unene kupita kiasi  na upungufu wa virutubishi vya vitamini na madini ndiyo unaoathiri zaidi sehemu kubwa ya jamii,” alisema Jane.

Alisema   utapiamlo huwaathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wsa umri wa uzazi.

“Mwili wa binadamu hauna uwezo wa kutengeneza virutubishi. Ukosefu wa virutubishi hivi mwilini husababisha njaa iliyofichika (hidden hunger) na huchangia kwa kiwango kikubwa katika kusababisha magonjwa na vifo  hususan kwa watoto  chini ya umri wa miaka mitano na  kina mama walio katika umri wa kuzaa.

“Vitamini na madini hufanya kazi mbalimbali mwilini kama vile kusaidia kuupatia mwili nguvu na joto, kuujenga na kuulinda dhidi ya magonjwa mbaliambali,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles