33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo awaonya wakurugenzi nchini

JAFONA JANETH MUSHI, ARUSHA

WAKURUGENZI watendaji wa halmashauri   nchini  na makatibu tawala wa mikoa na wilaya wametakiwa kushughulikia majanga yanayotokea katika maeneo yao haraka  vinginevyo watawajibishwa ikiwamo   kuchukuliwa hatua kali za  sheria.

Agizo hilo lilitolewa   mjini hapa jana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Suleiman Jafo.

Aliyasema hayo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya   Halmshauri ya Jiji la Arusha  ikiwa ni pamoja na Shule ya Msingi Kisimani  ambayo iliezuliwa na upepo mkali.

Jafo akiwa katika shuele hiyo, alionyesha kukerwa na utendaji kazi wa ofisa ununuzi wa halmashauri hiyo pamoja na Baraza la Wataalamu wa Jiji (CMT),  katika kushughulikia ukarabati wa madarasa  manne ya shule hiyo iliyoezuliwa na Desemba 4 mwaka jana.

“Nawaagiza wakurugenzi na Ma-RAS kote nchini, hii ni shule ya mwisho iliyokumbwa na maafa mimi kutembelea.

“Nikikuta kokote shule imepata majanga halafu mmekaa muda mrefu bila kushughulikia tatizo mtawajibishwa … kufanya hivyo mnaonyesha hamtoshi kwenye nafasi zenu,” alisema Jafo

Alimtaka Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd na timu ya wataalamu wa jiji hilo  kuandika maalezo kwa Waziri wa Tamisemi kwa nini ukarabati wa madarasa hayo umechelewa na kwa nini wasichukuliwe hatua.

“Ofisa ununuzi wenu hapa hatoshi inawezekana kazi nyingi anazichelewesha … huu ni uzembe wa hali ya juu na hauvumiliki, ingekuwa ni halmashauri ya vijijini ni sawa.

“Lakini hapa mjini na fedha zipo kwa nini mcheleweshe ukarabati?  Shule imeezuliwa Desemba leo ndiyo ukarabati unaanza?” alihoji Jaffo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles