25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Maud wa ‘Songi Songi’ kutua Dar

JESTINA ZAUYA, TUDARCo

Msanii raia wa DR Congo atayetamba na wimbo wa ‘Songi Songi’, Maud Elka anatarajiwa kutua Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2021 kwa ajili ya kufanya shoo yake mwenyewe  aliyoipa jina la  Songi Songi Tour.

 Maud amethibitisha kufanya shoo hiyo kupitia ukurasa wake wa Istagram.

Mwanamuziki aliyejizolea mashabiki wengi hapa nchini licha ya kuishi DR Congo, amesema ziara itakuwa ni pamoja na kutembelea vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Oktoba 5-12, mwaka huu.

Wimbo wa Songi Songi ni kati ya nyimbo pendwa na inayofanya vizuri hii inatokana na mtindo alioimba.

Ngoma hiyo iliyotoka miezi sita iliyopita imefanyiwa pia  remix na msanii mkongwe wa bongo fleva, Ali Kiba  aliyoitoa Julai, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles