KOCHA wa PSG, Mauricio Pochettino, amekana taarifa zilizosambaa zikidai kuna bifu kati ya mastaa wake, Kylian Mbappe na Neymar.
Ilielezwa kuwa Mbappe alikerwa na kitendo cha Neymar kutompa pasi katika mchezo wa walioifunga Montpellier mabao 2-0 wikiendi iliyopita.
Licha ya tofauti hiyo, wawili hao walionekana kumaliza tofauti zao katika mazoezi ya Jumatatu ya wiki hii, ambapo ipo picha inayowaonesha wakicheka pamoja.
“Hayo ni mambo madogo. Mara nyingi huwa inatokea kwa wachezaji wakubwa. Huwa wanashindana na kila mmoja anataka kushinda,” amesema Pochettino.