RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amekwaa kizingiti baada ya rufaa yake ya kutaka aondolewe hukumu ya kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kosa la kuidharau mahakama.
Mahakama Kuu nchini humo ndiyo iliyothibitisha kuwa rufaa ya Zuma imetupiliwa mbali, hivyo ataendelea kutumikia kifungo hicho alichohukumiwa Juni, mwaka huu.
Julai, mwaka huu, Zuma mwenye umri wa miaka 79 aliomba adhabu yake ya miezi 15 iangaliwe upya kwa kile alichodai umri wake mkubwa unamuweka kwenye hatari ya kupata Corona akiwa gerezani.
Mwanasiasa huyo aliiongoza Afrika Kusini kuanzia mwaka 2009 hadi 2018 lakini utawala wake huo ulikabiliwa na shutuma nyingi za vitendo vya rushwa.