Nashik, India
Wagonjwa wa Corona 22 waliokuwa wamelazwa hospitali nchini India wamepoteza maisha kwa ukosefu wa Oksijeni kulikotokana na kuvuja kwa gesi hiyo.
Tukio hilo lilitokea jana katika Hospitali ya Zakir Hussain iliyoko jijini Nashik, wakati gari la Oksijeni likijaza hewa hiyo kwenye tanki la akiba.
Hata hivyo, bado haijafahamika kilichosababisha hewa hiyo kuvuja na kushindwa kuwafikia wagonjwa waliokuwapo hospitalini hapo.
Lakini maafisa walisema hapakuwa na oksijeni kwenye mashine za kusaidia kupumua kwa takriban dakika 30, na hivyo kusababisha vifo vya wagonjwa.
“Tutataka kuchunguza suala hili na kuchua hatua,” Kamishna wa manispaa ya jiji Kailash Jadhav alisema.
Hospitali kote nchini India zinahangaika kuendelea kuwapatia wagonjwa oksijeni huku wanaoihitaji wakiendelea kuongezeka.