29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond: Tushindane kwa kazi siyo mambo yasiyofaa

Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’ amewataka wasanii wenzake ambao waliwai kuwa kwenye lebo yake ya wasafi kuiga mfano wake na msanii mwenzake Ali Salehe Kiba, ‘AliKiba’ kutofikishana polisi.

Akiongeo mapema leo, Diamond ameonyesha kuchukizwa na mambo yanayoendelea kati ya msanii wake, Rayvanny na aliyewahi kuwa msanii wa lebo hiyo Harmonize kupelekana Polisi.

Ikumbukwe, Harmonize na Rayvanny kesi yao ipo Polisi kutokana na Harmonize kushtaki kuwa anachafuliwa kwa baadhi ya picha zake za utupu kusambaa mitandaoni.

Harmonize aliwashitaki wote waliohusika kusambaza hizo picha huku akiwashuku Rayvanny, Baba Levo, Juma Haji na Paula mtoto wa Kajala na Kajala mwenyewe.

Aidha, Diamond amesema kuwa anachotaka kuona ni kusikia wanashindana kwenye kazi na sio mambo yasiyohusu kazi, huku akichomelea msumari wa mwisho kuwa yeye hakuwafundisha kupelekana Polisi.

“Sijafurahishwa kusikia wanapelekana Polisi, waige mifano ya sisi kaka zao mfano mimi na Alikiba hatukuwahi kuepelekana polisi tulikuwa tunashindana kupitia kazi zetu tu,” amesema Diamond

Ikumbukwe jana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilimesema linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa picha za utupu zikimuhusisha Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rajab Abdul Kahal maarufu kama Harmonize.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hadi sasa wamehojiwa Watu watano kuhusiana na sakata hilo na wapo nje kwa dhamana.

“Watuhumiwa hao ni Frida Kajala Masanja (36), Paula Paul Peter (18), Raymond Mwakyusa maarufu RayVanny (27), Claiton Revocuts maarufu Baba Levo (34), Catherine John na Juma haji (32)”amesema Mambosasa

“Watuhumiwa hawa wote walikamatwa, wakahojiwa na kwa vile dhamana ipo wazi wapo nje kwa dhamana na taratibu za upelelezi zinaendelea zikikamilika jalada litaenda kwa Wakili Mkuu wa Serikali na kama akiona kuna jinai watafikishwa Mahakamani,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles