25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanaume wanaopigwa wawekewe utaratibu wao- Dk. Gwajima

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameiagiza Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kuweka utaratibu wataalamu wanaume kutoka Idara hiyo kusikiliza na kupokea malalamiko ya wanaume wanaopigwa na kunyanyaswa.

Amesema sio kwamba wataalamu Wanawake hawawahudumii vizuri bali kusikilizwa na wanaume kunawafanya wawe huru kusema matatizo yao.

Akizungumza leo, Februari 2 na Waandishi wa Habari kuhusu vitendo vya ukatili katika jamii.

Waziri Dk. Gwajima amesema Wizara yake inataka ipate maoni ya kina baba wanaopigwa ili waweze kujua matatizo yao.

“Masuala ya wanaume yashugulikiwe na Wanaume naagiza Idara kuu wekeni wanaume katika kushughulikia matatizo hata kwenye choo kuna Me na Ke basi tufanye wahudumu wetu wawe mchanganyiko sisemi kwamba Wanawake hawawezi kusikiliza matatizo ya wanaume ile ni taaluma.

“Mambo ya kusikiliza mtu yanahitaji taaluma.Kwa wanaume sasa hivi nendeni kwa wanawake nendeni kwa wanaume ili tatizo lako liweze kutatuliwa,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles