33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kusitisha uagizaji wa vifaa vya kuunganishia gesi kutoka nje

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Serikali imesema, itasitisha uagizaji wa vifaa vinavyotumika kuunganisha na kusambaza gesi asilia, baada ya miezi sita kupita lengo likiwa ni vifaa hivyo kuzalishwa nchini.

Vifaa ambavyo serikali itapiga marufuku kuagizwa kutoka nje ya nchi  ni Koki,mabomba,vyuma vinavyotumika katika gesi asilia pamoja na mita.

Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani(Katikati) akiwa na Mgurugezni Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio(wakwanza kushoto) na viongozi wengine.

Akizungumza mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam katika kikao kilichoandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) ikilenga majadiliano na wazalishaji wa vifaa vinavyotumika kuasambaza na kuunganisha gesi asilia, Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani, amesema serikali imedhamiria kuzuia vifaa hivyo kuingizwa nchini ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa ndani kujenga viwanda.

Dk.Kalemani amesema, mahitaji ya vifaa hivyo ni mkubwa huku akieleza kuwa hatua ya kusitisha uagizaji nje  italeta changamoto kidogo lakini baadae kutakuwa na fursa nyingi ikiwemo kuongezeka kwa ajira,serikali kupata kodi  na miradi kutekelezwa kwa wakati

“Mahitaji yetu ni mabomba  ya miradi midogo ya gesi asilia ya kilometa 200 hadi 300, vyuma vya kilometa 300 hadi 400 na mita za Luku kwa ajili ya matumizi ya gesi asilia kati ya 8,000 hadi 10,000,” amesema Dk. Kalemani.

Amesema vifaa kutoka nje ya nchi vinachukua mwaka mmoja kufika nchini, hivyo mradi unaoweza kukamilika miezi mitatu, unachukua zaidi ya mwaka.

Dk.Kalemani amesema watengenezaji wa vifaa hivyo nchini watapata masoko katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta  kutoka Uganda mpaka Tanzania,

Aidha, amebainisha kuwa kuanzia mwakani, mikoa mitano itaanza kupelekewa gesi asilia, kwa kuwekwa kwenye matanki makubwa na kisha kujengwa miundombinu ya kuingiza ndani ya nyumba.

Amesema wataanza na nyumba za serikali katika Mji wa Serikali wa Mtumba, Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio amesema viwanda vitakavyozalisha bidhaa hizo nchini Tanzania, havitakuwa na masoko ya ndani pekee, bali na nje ya nchi katika miradi mikubwa ya kupeleka bomba la gesi Uganda, Msumbiji na Kenya na mradi mkubwa wa LNG utakaofungua fursa ya vifaa vingi kuhitajik

Miongoni mwa wadau walionyesha ari ya kutaka kujenga viwanda hivyo ambapo, Beatrice Charles kutoka Kiwanda cha Simba Plastic aliieleza kuwa kiwanda hicho wana uwezo wa kutengeneza mabomba ya kusafirisha gesi asilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles