MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ATANGAZA KUN’GATUKA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema anatarajia kustaafu kuiongoza benki hiyo mwaka 2019 ili kuwapa nafasi watu wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Dk. Kimei amesema ameiongoza benki hiyo tangu mwaka 1998 na atastaafu rasmi Mei 31 mwaka 2019.

“Mtu anapoondoka kwa ghafla kunakuwa na hisia mbalimbali lakini tunataka kuonyesha kwamba tunaandaa mrithi. Ni vizuri kuwapa nafasi wengine waendeleze hivyo nitabaki kuwa mwanahisa na mteja wa benki,” amesema Dk. Kimei.

Amesema wana wakurugenzi 25 waliowaandaa vizuri lakini mchakato wa kumpata mkurugenzi mtendaji mpya utahusisha pia watu wa nje ili kupata mtu atakayekuwa mzuri zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here