Na Victoaria Godfret, Dar es Salaam
Wagombea 24 wa nafasi mbalimbali wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya uongozi kwenye Shirikisho la Riadha Tanzania(RT).
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Januari 30, mwaka huu.
Ofisa Habari wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Najaha Bakari, amesema kati ya hao waliojitokeza wanaomba nafasi ya wajumbe ni zaidi ya 10, Makamu wa Rais wawili na Rais zaidi ya watatu.
Amesema bado milango ipo wazi kwa wadau wa riadha kujitokeza kuchukua fomu za kuomba nafasi za uongozi.
“Tunahitaji kupata wagombea wengi ili kupata ushindani na tuweze kupata uongozi makini utakaosaidia kuinua mchezo huo ufike mbali,” amesema Najaha.
Amesema mwisho wa kuchukua fomu na kurudisha Januari 26, mwaka huu, ameongeza kuwa zoezi la usaili kwa wagombea wote litafanyika Januari 28, mwaka huu.