24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

TAFF yazindua mpango mkakati

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Shirikisho la Soka kwa wenye Ulemavu Tanzania ( TAFF) limezindua Mpango Mkakati wa uwezeshaji wa timu ya Taifa ya Tanzania kuelekea kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia litakalofanyika 2022 nchini Uingereza.

Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya wanahabari (Media Centre) katika Uwanja wa Mkapa (zamani Taifa).

Akizungumza na wanahabari leo Januari 21, wakati akizindua mpango huo, Rais wa TAFF, Peter Sarungi, amesema kuwa malengo ni kuhakikisha wanafanya vyema na kishika nafasi ya kwanza hadi ya tatu kwenye mashindano hayo.

Amesema mpango huo umelenga kuunda taasisi imara ya kusimamia mchezo huo kuwaandaa viongozi, walimu, wachezaji waamuzi.

Sarungi amesema pia inalenga kuimarisha timu ya Taifa kwa kusaka vipaji mikoani, kushiriki mashindano ya kimataifa, kucheza mechi za kirafiki na kuandaa kambi ya muda mrefu.

Pia amesema kuwa utasaidia kutengeneza ajira kwa wachezaji wataonekana na kumpata fursa ya kucheza soka la Kulipwa.

“Tumeundambulisha leo mpango Mkakati wetu kwa wadau ili waweze kutambua na kujitokeza kuungana nasi katika kufanikisha malengo yetu, hivyo tunaomba sapoti,” alisema Sarungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles