24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

20 Percent: Kwanini nirekodie Afrika Kusini?

IMG_9548-960x640NA BEATRICE KAIZA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Abbasi Hamisi ‘20 Percent’, amesema hatofanya video nchini Afrika Kusini kama wafanyavyo wasanii wengine kwa kuwa kwa sasa video zake ni za uswahilini hazihitaji kufanyika nchini humo.

Msanii huyo aliyewahi kunyakua tuzo 5 za Kili alisema licha ya kuwa na uwezo wa kufanya video za nyimbo zake nchini humo, lakini kwa sasa bado hana wimbo unaohitaji video kutoka huko.

“Kwa sasa nina wimbo unaitwa ‘Mbaya hana Sababu’ ambao nitaufanyia hapa nchini na naamini video yake itakuwa bora na itafanya vizuri hata kama sitairekodia Afrika Kusini kama wafanyavyo wengine,” alisema 20 Percent.

Mkali huyo mwenye nyimbo za hisia aliongeza kwamba muziki wake si wa kushindana na msanii mwingine yeyote ndio maana hana haraka katika utoaji wa nyimbo zake pamoja na muziki wake.

“Mimi sishindani na mtu katika muziki wangu nafanya kama akili yangu inavyotaka na nyimbo zangu natoa ninapoona nipo tayari kutoa na si kushinikizwa na watu,” alieleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles