24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

15 mbaroni wakiuziana dhahabu Gesti

Na Derick Milton, Simiyu

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu 15 kwa kosa la kuuziana dhahabu katika nyumba ya kulala wageni (Guest House) katika mgodi wa dhahabu Lubaga namba mbili ulioko halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani humo.

Akiongea na Waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani humo Richard Abwao amesema kuwa watu hao wamekamatwa jana Januari 13, 2021 saa 1:00 jioni wakiwa na madini hayo yeney uzito wa gramu 9.2.

Abwao amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye nyumba hiyo (Guest) ndani ya mgodi huo wakifanya biashara ya kuuzia madini hayo kinyume cha sheria.

“Askari wetu wakiwa doria kwenye mgodi huo, walikuwakuta watu hawa wakifanya biashara hiyo kwenye nyumba ya kulala wageni ambayo ipo ndani ya mgodi huo, sheria inataka biashara ifanyike kwenye soko la madini.

“Na kwenye mgodi huo kuna soko la madini ambalo limeanzishwa na serikali linalotumika kuuzia madini, lakini hawa walikuwa sehemu ambayo siyo sahihi na lengo lao lilikuwa kukwepa kulipa kodi ya serikali,” amesema Abwao.

Awali, akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga amelipongeza jeshi hilo kwa kukamata watu hao, huku akibainisha kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho.

Kiswaga amesema kuwa serikali iliweka soko kwenye ngodi huo litumike kwa ajili ya kuuzia madini, ambapo ameeleza bado kuna watu wanaendelea kuuziana vichochoroni na kuwataka waache mara moja.

“Vyombo vyote vipo kazini, tutaendelea kuwakamata, tunazo taarifa wapo wengine, tutawakamata wote, niwaombe watu wote kwenye mgodi huo waache mara moja, hatutakuwa na mzaha kwenye hili,” amesema Kiswaga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles